Star Tv

Rais wa Shirikisho la Soka la Kenya Nick Mwendwa amekamatwa na maafisa wa polisi nchini humo.

Mwendwa amekamatwa na maafisa wa polisi waliovalia nguo za kiraia siku moja baada ya waziri wa Michezo Amina Mohamed kuvunja shirikisho hilo na kuunda kamati ya muda ya wanachama 15.

Jaji mstaafu Aaron Ringera aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo ambayo majukumu yake katika kipindi cha miezi sita ni pamoja na kuendesha masuala yote ya FKF.

Hatua hiyo inafuatia mapendekezo ya kamati ya ukaguzi aliyounda kuchunguza shirikisho la soka nchini humo linalokabiliwa na tuhuma za ufisadi na utawala mbaya na hata kufikia uamuzi wa kuvunja shirikisho hilo.

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.