Star Tv

Jenerali mwandamizi aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi hivi karibuni nchini Sudan, Abdel-Fattah Burhan, amejiteua tena kuongoza baraza tawala la mpito, ikiwa ni hatua inayoashiria nia yake ya kuimarisha udhibiti madarakani.

Miongoni mwa walioteuliwa ni watawala waliokuwa kwenye baraza lililopita, ikiwa ni pamoja na Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo, ambaye ni mshirika wa karibu wa Burhan aliyetajwa kuwa makamu wa rais, pamoja na majenerali wengine watatu waliorejeshwa.

Viongozi watatu wa makundi ya waasi pia wamejumuishwa kwenye baraza hilo na wawakilishi watano kutoka upande wa kiraia.

Hatua hii inachukuliwa licha ya ahadi zinazotolewa kila mara na watawala wa kijeshi kwamba watarejesha mamlaka kwa serikali ya kiraia, tangu mapinduzi ya Oktoba 25, ambayo yalifuatiwa na maandamano ya wanaounga mkono demokrasia wanaoshinikiza kurejeshwa kwa utawala huo wa kiraia.

#ChanzoDW

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.