Star Tv

Mwanzilishi wa mtandao wa wikileaks Julian Assange ameruhusiwa kufunga ndoa akiwa jela.

Julian Assange amepatiwa ruhusa ya kumuoa mpenzi wake Stella Moris katika jela ya Belmarsh.

Mwanzilishi huyo wa mtandao wa Wikileaks na Bi. Moris wana watoto wawili wa kiume, ambao alisema walipatikana wakati alipokuwa akiishi katika ubalozi wa Ecuador mjini London.

Huduma ya jela hiyo imesema kwamba ombi la Assange liliruhusiwa na gavana wa jela hiyo.

Wafungwa wana haki ya kuomba kufunga ndoa wakiwa jela chini ya kifungu cha ndoa cha 1983 na ombi hilo linaporuhusiwa wanapaswa kusimamia gharama zote za ndoa hiyo bila usaidizi wowote wa fedha za umma.

Katika mahojiano na gazeti la Mail la siku ya Jumapili mwaka uliopita, Bi Moris ambaye ni wakili wa Afrika Kusini, alifichua kwamba alikuwa katika uhusiano na Assange tangu 2015 na amekuwa akiwalea watoto wao wawili yeye binafsi.

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.