Star Tv

Watu wasiopungua 91 wamekufa nchini Sierra Leone baada ya lori la kubeba mafuta kulipuka katikati ya mji mkuu wa taifa hilo, Freetown.

Vyombo vya Habari kutoka nchini humo vimearifu kuwa miili ya watu 91 imepelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kinachosimamiwa na serikali na kuna ripoti kwamba idadi ya waliokufa huenda ni kubwa.

Picha na mikanda ya video inayosambaa kupitia mitandao ya kijamii imeonesha watu walioungua vibaya wakiwa wamelala kwenye mitaa ya mji wa Freetown huku moto ukiwa umeteketeza pia maduka na nyumba zilizokuwa karibu.

Mlipuko huo ulitokea baada ya lori la mafuta kugongana na gari lingine na miongoni mwa waathiriwa wa mkasa huo ni wale waliokimbilia kuchota mafuta.

Meya wa mji wa Freetown amesema madhara na hasara kamili ya ajali hiyo bado haijajulikana lakini polisi na maafisa wengine wa serikali wako eneo la tukio kutoa msaada unaohitajika.

#ChanzoDW

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.