Star Tv

Wafungwa wawili waliohukumiwa kunyongwa nchini Japan wamechukua hatua za kisheria dhidi ya hukumu waliyopewa ya kunyongwa siku moja.

Wafungwa wanaosubiri kunyongwa hujulishwa saa chache tu kabla ya kunyongwa, Ambapo hukumu ya kifo inafanywa kwa kunyongwa.

Wakili wao amesema, taarifa hiyo ya muda mfupi "haina utu kabisa", vyombo vya habari vya ndani nchini humo vimesema.

Makundi ya haki za binadamu yamekosoa hatua hiyo, wanasema inaathiri afya ya akili ya wafungwa.

"Wafungwa waliohukumiwa kifo wanaishi kwa hofu kila asubuhi kwa kuogopa kama siku itaisha,"- Alisema wakili wa wafungwa wote wawili Yutaka Ueda, kwa mujibu wa ripoti ya Reuters.

"Serikali imesema hii inakusudia kupunguza mateso kwa wafungwa kabla ya kunyongwa. Mataifa mengine, wafungwa wanapewa muda wa kutafakari mwisho wa maisha yao na kujiandaa kiakili."

Wafungwa hao waliwasilisha kesi katika mahakama ya wilaya katika jiji la Osaka siku ya Alhamisi, katika kile kinachoaminika kuwa cha kwanza, wakisema taarifa hiyo fupi haiwapi muda wa kuwasilisha kipingamizi chao.

Wafungwa hao wametaka fidia ya dola $193,500 wa mujibu wa wakili wao.

Kuna zaidi ya watu 100 wanaosubiri kunyongwa nchini Japan lakini hakuna hata mmoja aliyenyongwa takriban miaka miwili sasa.

#ChanzoBBCSwahili

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.