Star Tv

Polisi wa Kiislamu katika jimbo la Kano inayofahamika kama Hisbah imemkamata mwanaume mwenye umri wa miaka 26 kwa jina Aliyu Na Idris ambaye taarifa yake imekuwa ikienea kwenye mitandao ya habari ya kijamii wikiendi iliyopita kwa kutangaza kuwa anataka anunuliwe kutokana na "umasikini".

Kamanda wa Hisbah Harun Ibn Sina ameithibitishia BBC kukamatwa kwake, na kuongeza kuwa vitendo vya Aliyu Na Idris vimezuiwa.

"Ndio tulimkamata Jumanne na amekuwa pamoja nasi usiku, kile alichokifanya kinazuiwa katika Uislamu, huwezi kujaribu kujiuza hata uwe katika hali gani."

Fundi huyo wa nguo aliyekamatwa, alikuwa akizungumza na waandishi wa habari nchini Nigeria, akisema kwamba alikuwa na matatizo makubwa ya kifedha, ndio maana akaamua kujiuza kwa Naira Milioni 20 ($49,000; £35,000) ambayo ni bei aliyokuwa ameichapisha kwenye bango alilotembea nalo kwa mtu yeyote ambaye angempatia maisha yake yote.

"Nitawapa wazazi wangu Naira Milioni 10 ($24,000; £18,000)".

Pia nitalipa naira milioni tano kama kodi ya jimbo kama wataninunua ($12,000; £9,000), nitampatia Naira Milioni 2 ($5,000; £4,000) mtu aliyenisaidia kutangaza kuuzwa kwangu, na pesa zitakazobaki nitazitumia kufanya biashara kwa ajili ya kujikimu katika maisha yangu ya kila siku."

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.