Star Tv

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok.

Marekani imesema Waziri wake wa mambo ya nje Blinken, amezungumza kwa njia ya simu na Waziri Mkuu huyo aliyeondolewa madarakani, kufuatia Kiongozi huyo Abdalla Hamdok kurejea nyumbani.

Hamdok alikamatwa na kushikiliwa baada ya Jeshi kuendesha mapinduzi ya kiutawala siku ya Jumamosi.

Taarifa iliyotolewa inasema Blinken alikaribisha kuachiliwa kwa Hamdok na akarudia wito wake kwa wanajeshi wa Sudan kuwaachilia huru viongozi wote wa kiraia wanaoshikiliwa.

Maandamano ya kupinga mapinduzi hayo ya kijeshi yanaendelea, huku umati wa watu wakikusanyika katika mji mkuu wa Khartoum kuandamana na kufunga barabara.

Mapema, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan alitaka kuhalalisha mapinduzi hayo kwa kuwashutumu makundi ya wanasiasa kwa kuchochea raia dhidi ya vikosi vya jeshi.

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.