Star Tv

Serikali imesema malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni ya kupanda kwa bei ya nyama nchini yanaashiria ukuaji wa sekta hiyo ambapo wafugaji wameshauriwa kuwa huu ni muda mzuri kwa wao kuvuna na kuuza mifugo yao.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amebainisha hayo leo Octoba 20, 2021 jijini Dodoma, mbele ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utendaji kazi wa Bodi ya Nyama nchini mbele ya kamati hiyo.

Ulega amesema kipindi cha nyuma wafugaji walikuwa wakilalamika kutopata masoko ya mifugo yao ila katika kipindi cha sasa uhitaji wa mifugo katika viwanda vya kuchakata nyama nchini umekuwa mkubwa pamoja na hitaji la nyama katika soko la ndani.

“Sekta ambayo ulikuwa hauwezi kuisikia inasemwa, lakini leo inakuwa mjadala hivyo ni wakati mzuri sana kwa wafugaji kuvuna na kuuza mifugo yao.” Amesema Ulega

Amesema serikali imetengeneza uhitaji wa nyama baada ya kufungua biashara ya kuuza nyama nje ya nchi hali iliyosababisha uhitaji wa mifugo kwenye viwanda vya kuchakata hapa nchini kuongezeka.

Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya Nyama nchini Dkt. Daniel Mushi ameiambia kamati hiyo kuwa uhaba wa nyama uliojitokeza hivi karibuni na kusababisha bei ya nyama kupanda ni fursa ya kufuga kibiashara na kunenepesha mifugo hiyo.

Dkt. Mushi amesema kwa sasa sera ya serikali ni kuhamasisha uwepo wa vikundi kwa ajili ya unenepeshaji wa mifugo ili kupatikana kwa mifugo bora kulingana na hitaji la soko la sasa hususan kwenye viwanda vya kuchakata nyama nchini.

Kuhusu ugonjwa wa midomo na miguu (FMD) ambao unaathiri mifugo na kusababisha Tanzania kushindwa kupeleka nyama katika baadhi ya nchi za nje kulingana na masharti yaliyopo kwenye nchi hizo, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo, Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania (RVCT) Dkt. Bedan Masuruli amesema ugonjwa huo umekuwa ukiathiri kwa kiasi kikubwa biashara ya nje na kwamba umekuwa ukisababishwa na uwepo wa wanyama pori.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.