Jeshi la Uganda limezindua gari la kivita lililoundwa nchini humo.
Kamanda wa vikosi vya ardhi nchini Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ametoa taarifa ya uzinduzi wa gari hilo kwa kuweka picha katika ukurasa wake Twitter, picha ya kile anachosema kuwa gari la kwanza la kivita kutengenezwa nchini humo.
Anasema "liliundwa na kutengenezwa ncini Uganda", lakini hakutoa maelezo kuhusu muundo na gharama yake.
Gari hilo lililopewa jina la Chui lilizinduliwa na baba yake ambaye pia ndio Amiri Jeshi mkuu wa Taifa hilo, Rais Yoweri Kaguta Museveni.
Jeshi la Uganda mwaka jana lilihusika katika msako mkali dhidi ya maandamano yaliyotikisa mji mkuu, Kampala, kufuatia kukamatwa kwa mgombea urais Bobi Wine.
Maafisa wa Jeshi nchini humo walitetea utumizi wa silaha za moto, wakisema polisi na jeshi walikuwa wakikabiliana na waandamanaji.
#ChanzoBBCSwahili