Star Tv

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mkazi mmoja wa Kijiji cha Ndungi katika Wilaya ya Moshi kwa tuhuma za kumuua ndugu yake, William Shoo kwa madai ya kukataa kuchangia nyama ya Shilingi 1,500 waliyonunua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 11, 2021  amesema mauaji hayo yalitokea Oktoba 10, 2021 asubuhi baada ya marehemu kugoma kuchangia nyama hiyo waliyonunua.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, kabla ya mauaji hayo mtuhumiwa alinunua nyama kwa kushirikiana na marehemu ambapo walikula pamoja na walipomaliza kula marehemu alikataa kuchangia chochote ndipo ugomvi ukaanza.

Amesema katika ugomvi huo, mtuhumiwa alimkata ndugu yake na kitu chenye ncha kali kichwani na kusababisha kifo chake.

"Awali kabla ya tukio hilo, mtuhumiwa alinunua nyama kwa kushirikiana na mwenzake, ambayo ina thamani ya Shil. 1,500 walipokula pamoja ndugu yake huyo alikataa kulipia, ndipo ugomvi ukaanza ambapo ilipelekea kuchukua maamuzi hayo ya kumkata na kitu chenye ncha kali"

 

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.