Star Tv

Makamu wa Rais Dokta Philip Mpango amesema hajaridhishwa na shirika la Posta jinsi linavyotumia fursa za masoko ya nje ya nchi hususani jumuiya ya afrika ya mashariki na ukanda wa SADC kwani takwimu zinaonyesha kuwa huduma za Posta zinachangia chini ya asilimia 0.5 ya fedha za kigeni zinazotokana na mauzo ya huduma za Posta nje ya nchi

Makamu wa Rais Dkt. Mpango ametoa kauli hiyo wakati akihitimisha siku ya Posta duniani katika maadhimisho ya siku hiyo yaliyofanyika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini
Dodoma.

Dkt. Philip Isdor Mpango amesema Serikali inafurahi uwepo wa uhusiano mkubwa kati ya malengo makuu ya Umoja
wa Posta Duniani na malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na yale ya Sera ya Taifa ya Posta ya 2003 hasa katika kuwahudumia wananchi, lakini pia inapaswa kuendelea kuboresha huduma zake.

Akiwahutubia mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma, wageni kutoka sehemu mbalimbali na watoa huduma washiriki wa huduma za mawasiliano nchini, Dkt. Mpango amesema
Serikali imeshuhudia mageuzi makubwa ndani ya Shirika la Posta, kutokana na huduma mbalimbali zilizoanzishwa na shirika hilo zikiakisi matumizi ya teknolojia katika
kuwahudumia watanzania.

“Tumeshuhudia Posta ikibadilisha namna ya utoaji huduma zake kwa jamii kulingana na mahitaji na ndio maana leo hii tunashudia hatua ya Posta kuwa ya kidigitali na kuweza kuwafikia watu wengi kwa urahisi zaidi“. alisema Makamu wa Rais Dkt. Mpango


Mbali na kupongeza jitihada hizo Makamu wa Rais Dkt. Mpango amesema, kupitia Shirika la Posta Tanzania, Serikali inahitaji kuona utendaji wenye tija ikiwa ni pamoja na
kuwahudumia wananchi kwa ufanisi kupitia mtandao mpana wa Shirika la hilo lenye matawi zaidi ya 350 yaliyosambaa nchi nzima, bara na visiwani.

 “Ni muhimu taasisi hii iguse jamii kihuduma kwakuwa ilianzishwa ili kuhakikisha inatoa huduma kwa niaba ya Serikali na kuwahudumia wananchi wote bila kujali mahali
walipo"- Alibainisha Dkt. Mpango.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kijaji amesema Wizara yake imefanya maadhimisho hayo kwa siku nne mfululizo na
kushirikisha wadau mbalimbali katika Sekta ya Posta na nje ya Sekta ya Posta, nia ikiwa ni kuonesha Umma umuhimu wa huduma za Posta nchini.

Awali akizungumza katika kilele cha maadhimisho hayo ya siku ya Posta Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Rahma Kassim Ali
amesema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatoa hongera kwa umoja wa Posta duniani kwa kufikisha miaka 147 tangu kuanzishwa kwake akisema siku ya Posta duniani inabeba
dhana muhimu sana ya muungano.

“Hata kama hatuongei lugha moja lakini dunia nzima inaunganishwa na nguvu ya barua na mizigo inayowekwa stempu”. alisema, Rahma Kassim Ali.

Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU), Ndg. Sifundo Chief Moyo ambaye pia ameshiriki katika kilele cha maadhimisho hayo amesama PAPU itaendelea kushirikiana na nchi mwanachama za umoja huo katika kusambaza taarifa na miongozo pamoja na kufanya tafiti mbalimbali.

Kila Ifikapo Oktoba 9 ya kila mwaka, Tanzania kama mwanachama wa Posta duniani aliyejiunga mwaka 1963, huungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya umoja huo
ulianzishwa mwaka 1874.

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.