Star Tv

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amesema anajiuzulu siasa na hatagombea katika uchauzi wa mwaka ujao.

Bwana Duterte mwenye umri wa miaka 76 mwezi uliopita amesema kuwa hatagombea kiti cha makamu wa rais mwaka 2022.

Katiba ya nchi hiyo inawaruhusu marais kuhudumu muhula mmoja wa miaka sita pekee.

Lakini sasa anasema ameamua kujiondoa kwenye uchaguzi wa mwaka ujao kwani "hisia za Wafilipino wengi ni kwamba sifai".

Hatua hii inakuja huku kukiwa na uvumi kwamba binti yake anaweza kugombea urais.

Bwana Duterte, mtu mwenye utata na "mwenye nguvu ", aliingia mamlakani mwaka 2016 ambapo aliahidi kupunguza uhalifu na kutatua mzozo wa madawa ya kulevya nchini humo.

Lakini wakosoaji wanasema katika kipindi cha miaka mitano akiwa mamlakani, Bw Duterte amewachochea polisi kufanya mauaji ya ukiukaji wa sheria ya washukiwa katika kile alichokiita "vita dhidi ya mihadarati ".

Mwezi uliopita Bi Duterte-Carpio alisema kuwa hatajiunga na kinyang'anyiro cha kuwania urais kwasababu yeye na baba yake wamekubaliana kuwa ni mmoja kati yao tu atakayegombea katika uchaguzi ujao utakaofanyika mwezi Mei.

Tangazo la ghafla la kujiuzulu kwa Bw Duterte Duterte amelitoa akiwa mjini Manila katika eneo ambalo alikuwa anatarajiwa kujisajili kama mgombea.

Alisema kuwa kugombea kama Makamu wa rais " kutakuwa ni kukiuka katiba ya nchi ".

Msemaji wake Harry Roque, hatahivyo, hakuelezea kwamba Bw Duterte ataondoka kabisa katika siasa katika siku zijazo.

Bw Roque ameiambia BBC kuwa tangazo hilo "linamaanisha kuwa hana haja na kuwa Makamu Wa rais na kuhusu iwapo atajiuzulu kabisa na kutoka katika siasa, nitahitaji kupata thibitisho la hili kutoka kwake".

Ana mtindo wa kusema mambo yanayofanana na hayo, na baadaye kugeuza usemi wiki moja baadaye.

Mwezi Septemba 2015, katika kampeni za kuelekea uchaguzi, aliyekuwa meya wa Davao wakati huo alisema alikuwa amepanga "kujiuzulu maisha ya umma daima ".

#ChanzoBBCSwahili

Latest News

Dkt. Jafo ofisi yake, imekamilisha taratibu zote za kupata Ithibati ya Kitabu ch...
24 Apr 2023 09:38 - Kisali Shombe

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewasilisha bungeni Hotuba ya Ma [ ... ]

TARI, Ukiruguru kuzindua Kifaa cha kupandia Mbegu cha Rafiki
23 Apr 2023 18:33 - Kisali Shombe

Sekta ya Kilimo ni mhimili wa uchumi wa Tanzania na imekuwa ikichangia Pato la mkulima mmoja mmoja, kaya na Taifa kwa uj [ ... ]

Wanawake kuwa sehemu ya Elimu dhidi ya Itikadi Kali na Ugaidi Afrika.
17 Apr 2023 10:28 - Kisali Shombe

Mnamo Oktoba 14, 2017, Mogadishu, Somalia ilikumbwa na shambulio baya la kigaidi lililoua watu 587 na kujeruhi zaidi ya  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.