Star Tv

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshiriki mazishi ya aliyekuwa Mbunge Ngorongoro na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji, William Tate Ole Nasha na amewasihi wananchi wamuenzi kwa kuyaendeleza mambo mazuri yote aliyofanya enzi za uhai wake.

Waziri Majaliwa ambaye ameshiriki mazishi hayo kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan amesema kifo cha Ole Nasha ni pigo kubwa kwa upande wa Serikali, Cham Cha Mapinduzi (CCM), Bunge pamoja na kwa wanafamilia na wananchi wa Ngorongoro.

Mazishi hayo ya Ole Nasha yamefanyika leo (Jumamosi, OktobA 2, 2021) nyumbani kwake katika kijiji cha Osinoni kata ya Kakesyo wilayani Ngorongoro mkoa wa Arusha.

Mbunge huyo alifariki Jumatatu, Septemba 27, 2021 mkoani Dodoma.

Waziri Mkuu amesema Rais Samia anawataka Watanzania waenzi mambo mazuri yote aliyoyafanya marehemu Ole Nasha ili jamii aliyokuwa anaiongoza inufaike. “Marehemu amefanya mambo mengi na ametoa mchango wa hali ya juu kwa Serikali.”-Amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Aidha, amesema jambo la muhimu kwa sasa ni kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema; “Mke wa marehemu, watoto, ndugu, jamaa na wabunge namuomba Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu.”

Kwa upande wake, Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu –Uwekezaji, Geofrey Mwambe amesema Ofisi ya Waziri Mkuu imepata pigo kubwa kwa kumpoteza mpiganaji kwa sababu marehemu Ole Nasha alikuwa mtumishi hodari.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, viongozi wa Serikali, wabunge pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.