Star Tv

Korea Kaskazini imesema kuwa imefanyia majaribio kombora jipya la kupambana na ndege siku ya Alhamisi, hili likiwa la nne kujaribiwa chini ya mwezi mmoja.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken amesema jaribio hilo "linabuni mazingira mabaya ya kukosekana kwa utulivu na usalama".

Pyongyang inasema kuwa inahitaji silaha zake kujilinda, ikishtumu Marekani na Korea Kusini kwa "unafiki".

Majaribio ya hivi karibuni ya silaha za Korea Kaskazini yanaonyesha kuwa nchi hiyo inaongeza mpango wake wa silaha.

Kulingana na shirika la habari la serikali KCNA, kombora hili jipya la kupambana na ndege lilionyesha "utenda kazi mzuri mzuri na pia ni mamoja ya "teknolojia mpya muhimu".

Marekani imekuwa ikitoa wito kwa Korea Kaskazini kuachana na uundaji silaha za nyuklia, huku uhusiano wa Pyongyang na utawala wa Rais Joe Biden kufikia sasa ukikumbwa na mvutano.

Mwezi uliopita shirika la atomiki la Umoja wa Mataifa lilisema Korea Kaskazini huenda ilianzisha tena mtambo ambao unaweza kuzalisha madini ya Plutonium ambayo hutumika kutengeza silaha za nyuklia, na kuiita maendeleao "yanayosumbua sana".

Jaribio la kombora hili jimpya linakuja siku moja baada ya Rais Kim Jong-un kuashiria kuwa anataka kuregesha mawasiliano muhimu kati ya nchi hiyo na majirani zao wa Kusini.

Bwana Kim hata hivyo, alishutumu Marekani kwa "kupigia debe ushirikiano wa kidiplomasia"..... lakini yote ni njama ya kudanganya jamii ya kimataifa na kuficha vitendo vyake vya uhasama"

Baadhi ya wachambuzi wanaamini hatua ya Pyongyang inalenga kusambaratisha uhusiano kati ya Washington na Seoul kwa kuendeleza mawasiliano na Korea Kusini na kutenga Marekani.

#ChanzoBBCSwahili

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.