Star Tv

Serikali imetoa Shilingi Milioni 700 kusaidia ukarabati wa barabara za vijijini katika jimbo la Karagwe mkoani Kagera ili kuboresha miundombinu ya jimbo hilo hatua inayosaidia kurahisisha mawasiliano na kuboresha huduma za kijamii jimboni humo.

Akiwa ziarani jimboni humo kukagua miundombinu ya barabara zinazokarabatiwa, Mhe. Innocent Bashungwa amesema fedha zilizotolewa kwa ajili ya ukarabati wa barabara jimboni humo zitumike kulingana na malengo yaliyokusudiwa kwa kuzingatia matumizi sahihi ya fedha zilizotolewa.

Bashungwa amewahimiza wabunge wenzake mkoani Kagera kuwa mstari wa mbele kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili fedha iliyotolewa na Serikali kwa ajili ya kuboresha barabara za vijijini zifanye kazi iliyokusudiwa kufikia malengo ya kuwahudumia wananchi kwa kuboresha uchumi wao na taifa kwa ujumla.

“Sisi tunamshukuru Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kutupa kiasi hiki kikubwa cha fedha ili tuboreshe barabara kwenye majimbo yetu lakini wito wangu ni kwamba hawa wataalumu wasisubiri mbunge aende site ili kuwaambia eneo fulani mlitakiwa muweke mataleo au mitaro ya maji ili yasiaharibu barabara, wataalamu wenyewe wanatakiwa wajue tangu wanaposanifu ujenzi husika” alisema Mhe. Bashungwa.

Akizungumzia hatua hiyo meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA wilaya ya Karagwe Bw. Kalimbula Malimi amesema baada ya ziara hiyo sehemu zote zilizoainishwa ambazozinahitaji marekebisho zitafanyia kazi haraka iwezekanavyo.

Katika ziara hiyo Bashungwa aliambatana na Madiwani wa kata mbalimbali, watendaji wa TARURA na TANROAD ambapo ameeleza kushtushwa kwake na namna mkandarasi anayetekeleza ukarabati wa barabara yenye urefu wa kilometa 96 inaanzia kata ya Nyakahanga kwenda kata za Nyabiyonza, Bweranyange, Nyakakika, Nyakabanga, Kibondo mpaka Lukanja ambayo imejengwa bila kuweka matoleo ya maji na mitaro ya barabara.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa wilaya ya Karagwe akiwemo diwani wa kata ya Nyakakika Exsavery Buguzi wameeleza matarajio yao kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutaongeza urahisi wa shughuli za biashara kwa maana ya usafiri na kusafirisha mizigo kati ya wakazi wa mkoa wa Kagera na nchi jirani ya Rwanda kupitia kivuko cha Bweranyange ambacho kinaziunganisha nchi hizo mbili kwa usafiri wa majini.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.