Star Tv

Polisi katika jimbo la Nigeria la Lagos wamemtia nguvuni mwanaume mmoja kwa madai ya kuyaondoa matiti ya binti yake mwenye umri wa miaka minane kwa kutumia jiwe la moto.

Rekodi ya polisi inasema kuwa baba huyo alitekeleza maasi dhidi ya binti yake, kwasababu matiti yake yalikuwa yameanza kuonyesha 'chuchu', ambazo ni ishara za kwanza za kubalehe.

Kwa sasa msichana huyo amelazwa hospitalini kwa matibabu, huku ripoti zikisema kuwa yuko katika hali mahututi, kutokana na majeraha aliyosababishiwa na baba yake mzazi Bwana Banjo.

Baba yake msichana huyo aliripotiwa polisi na kikundi cha kutetea haki za watoto, na Msemaji wa polisi wa jimbo la Lagos DSP Asijebotu amethibitisha madai hayo, akisema kuwa wanafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Kulingana na taarifa nchini Nigeria, wazazi wa msichana huyo kwa sasa wanashikiliwa na polisi katika jimbo la Lagos.

Mkuu wa kikundi cha kutetea haki za watoto Comrade Ebenezer Omejalile, ambacho kilimshitaki baba huyo, ameiambia BBC kwamba Bwana Banjo, anayefahamika kama Panel, "Aliyabana na kisha kuyachoma matiti ya binti yake."

"Baba wa msichana huyo alitumia jiwe la moto alilolifunga ndani ya nguo na kumchoma hadi alipohakikisha kuwa ameyaharibu kabisa matiti ya binti yake," alisema.

Alisema pia kwamba baba huyo alielezea kutoridhishwa kwake na jinsi binti yake alivyokuwa ameanza kuonyesha dalili za saratani ya matiti kwenye matiti yake, na ndio maana alitaka kuyazuia yasiote.

Aidha, Mama yake msichana huyo alisema kuwa mumewe amekuwa akimpiga binti yake mara kwa mara.

#ChanzoBBCSwahili

 

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.