Star Tv

Waziri wa Maji Jumaa Aweso ametoa rai kwa wabunge hapa nchini kuziomba mamlaka zinazowazunguka kuboresha miundombinu ya michezo ikiwa ni pamoja na viwanja vya michezo katika maeneo yao ili kuwa katika viwango vinavyotakiwa.

Aweso amefafanua kwamba endapo viwanja vya michezo vitakuwa katika viwango vinavyotakiwa, hali hiyo itawafanya vijana wengi kushawishika kushiriki michezo mbalimbali.

Rai hizo amezitoa jana (Septemba 12) wakati akihitimisha ligi ya Bashungwa Cup iliyokuwa ikizishirikisha timu 23 kutoka kata 23 za Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

Kauli ya Waziri Aweso inafutia ombi la wakazi wa wilaya ya Karagwe waliozungumza kwa nyakati tofauti tofauti wakiomba Halmashauri ya wilaya hiyo kuufanyia ukarabati uwanja wa mpira wa Kayanga ili uwe na viwango vya kuruhusu mashindano makubwa ya ngazi ya mkoa na hata taifa kufanyika uwanjani hapo.

Akizungumza katika fainali hizo mwandaaji wa mashindano hayo ambaye ni mbunge wa Jimbo la Karagwe na Waziri anayesimamia sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono jitihada za kukuza michezo katika safari ya kukuza vipaji vya vijana.

“Wote tunaamini kwenye umoja, ninamaanisha tukiungana tunaweza, Serikali inafanya kila kinachowezekana kukuza sekta ya michezo nchini, lakini si dhambi kwa mdau yeyote kutuunga mkono popote unapoweza katika kutimiza ndoto ya vijana wetu wenye vipaji vya michezo.” Alisema Waziri Bashungwa.

Fainali hiyo iliyozikutanisha timu mbili ambazo ni Bugeni FC na Nyabiyonza FC zote za wilayani Karagwe.

Timu ya Bugene FC imeibuka mshindi kwa mikwaju ya penaliti na kubeba kombe pamoja na zawadi ya shilingi milioni mbili na laki tano huku timu ya Nyabiyonza ikishika nafasi ya pili na kubeba kitita cha shilingi milioni moja laki mbili na elfu 50, huku mshindi wa tatu ambaye ni Kihanga FC akiibuka na shilingi laki saba na elfu hamsini.

Mashindano ya Bashungwa Cup yalizinduliwa rasmi mwaka 2017 na yamekuwa yakiwakutanisha vijana kila mwaka kushindania zawadi mbalimbali, lengo likiwa ni kuwaunganisha wakazi wa wilaya ya Karagwe na kuibua vipaji vya vijana kupitia mchezo wa soka.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.