Star Tv

Rais wa zamani wa Afghanistan Ashraf Ghani ameomba msamaha kwa watu wa Afghanistan baada ya kukimbilia katika nchi za Falme za Kiarabu.

Rais Ghan amewaambia raia wake kuwa ilimbidi afanye maamuzi magumu; "Kuondoka Kabul ulikuwa uamuzi mgumu zaidi maishani mwangu," amesema, akiongeza kuwa anajuta kwamba "hakuweza kumaliza hilo kwa njia tofauti."

Bwana Ghani aliondoka ghafla nchini Afghanistan wakati wanamgambo wa Taliban walipokuwa wakiendelea kuingia kwenye mji mkuu mnamo Agosti 15.

Alisema hakuwa na nia ya kuwaacha watu wake lakini "ilikuwa ndio njia pekee iliyosalia."

Katika taarifa iliyoshirikishwa kwenye mtandao wa Twitter siku ya Jumatano, Bw. Ghani alisema hakuwa na njia nyingine yoyote zaidi ya kuondoka nchini humo ili kuepusha kuenea kwa ghasia.

"Niliondoka kwa kushawishiwa na usalama wa ikulu, ulionishauri kuwa kuendelea kuwepo kulihatarisha kutokea kwa mapigano mitaani na katika barabara za mji kama ilivyotokea wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka ya 1990,"- aliandika, akiongeza kuwa alifanya hivyo "kuokoa mji wa Kabul na raia wake Milioni sita".

Alisema alikuwa amejitolea kwa kipindi cha miaka 20 kusaidia Afghanistan kuwa "nchi ya kidemokrasia, mafanikio na huru."

Bwana Ghani ameongeza kuwa alikuwa na "masikitiko makubwa" kwamba "muda wangu mwenyewe uliishia kwa majuto kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wangu."

Latest News

KENYA YAPIGA MARUFUKU FILAMU YA WAPENZI WA JINSIA MOJA.
23 Sep 2021 14:44 - Grace Melleor

Bodi ya Filamu Kenya inasema kuwa filamu kuhusu maisha ya wanandoa wa jinsia nchini Kenya imepigwa marufuku nchini humo. [ ... ]

SHIL. MIL. 700 ZATOLEWA KUKARABATI BARABARA KARAGWE.
23 Sep 2021 13:55 - Grace Melleor

Serikali imetoa Shilingi Milioni 700 kusaidia ukarabati wa barabara za vijijini katika jimbo la Karagwe mkoani Kagera il [ ... ]

BABA AKAMATWA KWA KUCHOMA 'MATITI' YA BINTI YAKE.
22 Sep 2021 13:32 - Grace Melleor

Polisi katika jimbo la Nigeria la Lagos wamemtia nguvuni mwanaume mmoja kwa madai ya kuyaondoa matiti ya binti yake mwen [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.