Star Tv

Watafiti wanachunguza aina mpya ya virusi vya corona nchini Afrika Kusini, Ambapo Virusi hivyo aina ya C.1.2 huzaana mara mbili zaidi lakini havijatajwa kuwa vyenye kutia wasiwasi.

Matukio ya virusi hivyo yamerekodiwa katika kila mkoa nchini Afrika Kusini pamoja na mataifa saba ya Afrika, bara Asia, Ulaya na maeneo ya Oceania.

Wanasayansi wanatathmini jinsi aina hiyo ya virusi inavyokabiliana na viini vinavyopigana na corona. Pia wanachunguza jinsi vinavyozaana na maambukizi yake.

Maria van Kerkhove, afisa wa kiufundi anayeongoza uchunguzi huo kwa niaba ya shirika la la Afya duniani WHO amesema kwamba virusi hivyo havionekani vikiongezeka.

Amesema kwamba aina hiyo ya virusi ndio inayoendelea kuwaathiri wengi na kwamba WHO itaufahamisha umma iwapo kutakuwa na mabadiliko yoyote.

Afrika kusini ni taifa ambalo limeathiriwa vibaya na aina zote mbili za ugonjwa wa UVIKO-19 ikiwemo yale ya virusi vya Delta na Beta ambayo yanasambazwa kwa urahisi zaidi na taifa hilo limesajili maambukizi 2,770,575 ya virusi vya corona ikiwemo vifo 81,830.

Latest News

KENYA YAPIGA MARUFUKU FILAMU YA WAPENZI WA JINSIA MOJA.
23 Sep 2021 14:44 - Grace Melleor

Bodi ya Filamu Kenya inasema kuwa filamu kuhusu maisha ya wanandoa wa jinsia nchini Kenya imepigwa marufuku nchini humo. [ ... ]

SHIL. MIL. 700 ZATOLEWA KUKARABATI BARABARA KARAGWE.
23 Sep 2021 13:55 - Grace Melleor

Serikali imetoa Shilingi Milioni 700 kusaidia ukarabati wa barabara za vijijini katika jimbo la Karagwe mkoani Kagera il [ ... ]

BABA AKAMATWA KWA KUCHOMA 'MATITI' YA BINTI YAKE.
22 Sep 2021 13:32 - Grace Melleor

Polisi katika jimbo la Nigeria la Lagos wamemtia nguvuni mwanaume mmoja kwa madai ya kuyaondoa matiti ya binti yake mwen [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.