Star Tv

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amesema serikali itashirikiana bega kwa bega na majimbo ya Magharibi mwa Ujerumani yaliyoathirika kwa mafuriko ili kuzijenga upya jamii.

Akizungumza baada ya kuzuru mji wa Schuld, moja ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko, Merkel aliielezea hali katika maeneo hayo kuwa ya kutisha.

Merkel ambaye ameahidi msaada wa haraka wa kifedha, pia alizipongeza juhudi za uokozi zinazoendelea na mshikamano aliyouona wakati wa ziara hiyo, lakini akaonya kwamba shida kwenye eneo hilo hazitotatuliwa haraka.

Alisema kinachohitajika sasa ni sera inayozingatia maumbile na mabadiliko ya tabianchi kuliko ilivyofanyika katika miaka ya hivi karibuni.

Maafa hayo yamesababisha vifo vya watu 160 ikiwa ni 112 katika wilaya ya Ahrweiler iliyoko kwenye jimbo la Rhineland Palatinate. Watu wengine 700 wamejeruhiwa. Vifo vingine 48 vimeripotiwa katika jimbo jirani la North-Rhine Westphalia.

#ChanzoDWSwahili

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.