Star Tv

Mawaziri wa fedha kutoka kundi la mataifa 20 yaliyostawi na yanayoinukia kiuchumi kote ulimwenguni G20, wameidhinisha mkataba wa kihistoria wa kubadilisha mfumo wa kuyatoza ushuru mashirika ya kimataifa na kuzihimza nchi ambazo hazikushiriki kujiunga katika mkataba huo.

Mageuzi hayo yanayojumuisha ushuru wa kiwango cha chini cha asilimia 15 kwa mashirika ya kimataifa, yalikubaliwa na mataifa 131 mapema mwezi huu.

Lakini kuidhinishwa kwa mageuzi hayo na mataifa 19 yalioimarika zaidi kiuchumi pamoja na Umoja wa Ulaya kutasaidia kuhakikisha yanaanza kutekelezwa baada ya miaka mingi ya majadiliano.

Katika taarifa ya mwisho iliyotolewa na mawaziri hao baada ya mkutano wa siku mbili ulioandaliwa mjini Venice na Italia inayoshikilia urais wa kundi hilo la G20, wamesema kuwa wamefikia makubaliano ya kihistoria kuhusu mfumo thabiti na bora zaidi utakaosimamia ushuru wa kimataifa.
#ChanzoDWSwahili

Latest News

“MAISHA HAYAJI MARA MBILI, TUSIPOTOSHE KUHUSU CHANJO”-IGP. Simon Sirro.
29 Jul 2021 11:30 - Grace Melleor

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP. Simon Sirro, amewataka Wananchi na Watanzania kwa ujumla wasidanganywe na watu wacha [ ... ]

“MIMI NI MAMA, BIBI, MKE NA RAIS, SIWEZI KUJIWEKA KATIKA HATARI”-Rais Samia....
28 Jul 2021 10:26 - Grace Melleor

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokea chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19, Ambayo ameizindua leo Julai 28, Katik [ ... ]

MSICHANA AUAWA KWA KUVAA JEANS.
28 Jul 2021 09:51 - Grace Melleor

Msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Neha Paswan, mwenye umri wa miaka 17, anadaiwa kupigwa hadi kufa na watu wa fam [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.