Star Tv

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma, aliyetakiwa kujisalimisha gerezani ili kukitumikia kifungo cha miezi 15 kwa kuupuza amri ya Mahakama, amesema hatotii hukumu hiyo.

Wiki iliyopita, Mahakama ya Katiba ilimpa adhabu hiyo rais Zuma, kwa kutoheshimu agizo la Mahakama kutoa ushahidi kwa Tume iliyokuwa inachunguza madai ya ufisadi alipokuwa rais kati ya mwaka 2009 hadi 2018.

Akizungumza katika mkoa wa Kwa-Zulu Natal alikozaliwa, Zuma amewafananisha Majaji walitoa hukumu dhidi yake kama viongozi waliongoza taifa hilo wakati wa kipindi cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Kiongozi huyo amesema kumtaka aende jela kwasasa ni sawa na kumpa hukumu ya kifo; "Hakuna haja ya mimi kwenda jela, kunifunga katika kipindi hiki, kwa umri wangu, ni sawa na kunipa hukumu la kifo"- Alisema Zuma.

Zuma mwenye umri wa miaka 79, alipaswa kujisalimisha gerezani siku ya Jumapili wiki iliyopita, lakini Mahakama imekubali kusikiliza rufaa ya kupinga kifungo hicho cha miezi 15.

Aidha wafuasi wa Zuma wameapa kutokubali kiongozi wao huyo wa zamani kufungwa.

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.