Star Tv

Jeshi la Syria limedaiwa kuwaua watu nane kutokana na mashambulizi ya mizinga yaliyokuwa yakifanywa na jeshi hilo katika ngome ya waasi wa Idlib.

Watoto 6 ni miongoni mwa watu wanane waliouwawa na mashambulizi ya mizinga ya jeshi la Syria huko katika ngome kubwa ya mwisho ya waasi ya Idlib kaskazini/magharibi mwa taifa hilo.

Kwa mujibu wa shirika la uangalizi wa haki za binaadamu la Syria lenye maskani yake mjini London, Uingereza limesema mashambulizi hayo yamefanyika Asubuhi ya leo Julai 03, na  yanatajwa pia kuwajeruhi watu wengine 16 katika maeneo kadhaa Jabal al-Zawiya kusini mwa ngome hiyo.

Miongoni mwa waliuawa ni pamoja na watu watano wa familia moja, mume, mke na watoto wao watatu, mkasa huo umetokea kijiji cha Iblin, watoto wawili wameuwawa kijiji cha Balyun na mwingine kijiji cha Balshun.

Vifo hivi vya leo vinaelezwa kuwa ni vya viwango vya juu zaidi tangu kuanza kutekelezwa makubaliano ya kimataifa ya kusitisha mapigano ya Machi 2020, yenye lengo la kuilinda ngome hiyo yenye kudhibitiwa na waasi wenye itikadi kali dhidi ya mashambulizi ya serikali.

Latest News

“MAISHA HAYAJI MARA MBILI, TUSIPOTOSHE KUHUSU CHANJO”-IGP. Simon Sirro.
29 Jul 2021 11:30 - Grace Melleor

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP. Simon Sirro, amewataka Wananchi na Watanzania kwa ujumla wasidanganywe na watu wacha [ ... ]

“MIMI NI MAMA, BIBI, MKE NA RAIS, SIWEZI KUJIWEKA KATIKA HATARI”-Rais Samia....
28 Jul 2021 10:26 - Grace Melleor

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokea chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19, Ambayo ameizindua leo Julai 28, Katik [ ... ]

MSICHANA AUAWA KWA KUVAA JEANS.
28 Jul 2021 09:51 - Grace Melleor

Msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Neha Paswan, mwenye umri wa miaka 17, anadaiwa kupigwa hadi kufa na watu wa fam [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.