Star Tv

Pasi maalumu ya Umoja wa Ulaya, itakayoanza kutumika tarehe 1 mwezi Julai kurahisisha safari kwenda Ulaya kwa wale waliopata chanjo itaanza kufanya kazi lakini ikiwa na sharti moja muhimu.

Mtu yeyote aliyepewa chanjo ya AstraZeneca inayozalishwa na Taasisi ya Serum ya India hatastahiki kupata pasi hiyo, na hiyo inajumuisha raia wengi wa nchi za kipato cha chini na cha kati ambao walipatiwa chanjo zilizosambazwa na mpango wa COVAX uliofadhiliwa na WHO.

Hii ni kwasababu pasi maalumu ya Umoja wa Ulaya itatambua tu toleo la Vaxzevria la chanjo ya AstraZeneca ambayo ilitengenezwa nchini Uingereza au maeneo mengine ya Ulaya, na hivyo kupitishwa na Wakala wa Dawa wa Ulaya (EMA).

Aidha, Kwa upande mwingine, ununuzi na usambazaji mkubwa wa chanjo chini ya mpango wa COVAX unahusisha chanjo ya AstraZeneca, iliyotengenezwa na Taasisi ya Serum ya India.

Latest News

“MAISHA HAYAJI MARA MBILI, TUSIPOTOSHE KUHUSU CHANJO”-IGP. Simon Sirro.
29 Jul 2021 11:30 - Grace Melleor

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP. Simon Sirro, amewataka Wananchi na Watanzania kwa ujumla wasidanganywe na watu wacha [ ... ]

“MIMI NI MAMA, BIBI, MKE NA RAIS, SIWEZI KUJIWEKA KATIKA HATARI”-Rais Samia....
28 Jul 2021 10:26 - Grace Melleor

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokea chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19, Ambayo ameizindua leo Julai 28, Katik [ ... ]

MSICHANA AUAWA KWA KUVAA JEANS.
28 Jul 2021 09:51 - Grace Melleor

Msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Neha Paswan, mwenye umri wa miaka 17, anadaiwa kupigwa hadi kufa na watu wa fam [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.