Star Tv

Wazazi wawili wa watoto wa shule waliotekwa nyara katika eneo la Tegina katika jimbo la kati la Nigeria la Niger wamekufa kutokana na mshtuko, vimesema vyombo vya habari.

Wazazi hao walipatwa na mshtuko baada ya kupata taarifa ya genge la watu kuwateka wanafunzi kutoka kwenye shule yao Jumapili.

Wazazi hao walisemekana waliugua ghafla na kupoteza fahamu.

Watekaji nyara wanasemekana kuwa wamekuwa wakiwaomba kikombozi kabla ya kuwachilia watoto wao na wametishia maisha yao iwapo hawatalipwa, kulingana na taarifa.

Awali, Mkuu wa shule ya kiislamu aliiambia BBC kwamba alizungumza na watekaji nyara na wakamuhakikishia kuwa watoto walikuwa wazima na wenye afya.

Abubakar Alhassan alisema kuwa wanafunzi 136 hawajulikani walipo, wakiwemo watoto wake watano, baada ya kuhesabu idadi ya watoto kufuatia utekaji huo.

Aidha, Walimu watatu pia hawajulikani walipo. Hata hivyo, bado hakuna taarifa rasmi ya idadi kamili ya wanafunzi waliotekwa nyara. 

Latest News

WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KULIPA KODI BILA KUCHOKA.
14 Jun 2021 19:01 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kuendelea kujitoa kulipa kodi ili kuwez [ ... ]

WAZIRI MKUU MPYA AAPA KUIUNGANISHA ISRAEL.
14 Jun 2021 06:33 - Grace Melleor

Waziri Mkuu mpya wa Israel Naftali Bennett ameapa kuliunganisha taifa hilo ambalo linalezwa kufadhaishwa na chaguzi nne  [ ... ]

RAIS SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU NA JENGO LA BOT.
13 Jun 2021 14:11 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua kiwanda cha kusafisha dhahabu jijini Mwanza kinach [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.