Star Tv

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limeanza kikao maalum leo kuhusu Israel ambapo Mkuu wa haki za bindamu wa Umoja huo Michelle Bachelet amesema mashambulizi mabaya ya Israel dhidi ya Gaza huenda yakawa yamesababisha uhalifu wa kivita ikiwa yatabainika yalipindukia mipaka.

Kikao hicho kimeitishwa kutokana na ombi la nchi za kiislamu.Kikao hicho kinafanyika baada ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken kumaliza ziara yake mashariki ya kati na leo alhamisi ameelekea nyumbani Marekani.Kituo chake cha mwisho kilikuwa Jordan ambako alitowa mwito wa ushirikiano wa kikanda kuimarisha makubaliano ya kusitisha vita baina ya Israel na wanamgambo wa Gaza. Kadhalika waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani jana alikutana na rais wa Misri AbdelFatah al Sisi mjini Cairo ambapo alimpongeza kwa kusaidia kumaliza vita vikali. Wizara ya afya mjini Gaza imesema mashambulizi ya anga ya wanajeshi wa Israel yaliyofanywa dhidi ya Gaza yaliwauwa wapalestina 254 wakiwemo watoto 66 na watu 1,900 walijeruhiwa kufuatia siku 11 za vita.

 

CHANZO: IDHAA YA KISWAHILI (DW)

 

 

 

 

Latest News

WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KULIPA KODI BILA KUCHOKA.
14 Jun 2021 19:01 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kuendelea kujitoa kulipa kodi ili kuwez [ ... ]

WAZIRI MKUU MPYA AAPA KUIUNGANISHA ISRAEL.
14 Jun 2021 06:33 - Grace Melleor

Waziri Mkuu mpya wa Israel Naftali Bennett ameapa kuliunganisha taifa hilo ambalo linalezwa kufadhaishwa na chaguzi nne  [ ... ]

RAIS SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU NA JENGO LA BOT.
13 Jun 2021 14:11 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua kiwanda cha kusafisha dhahabu jijini Mwanza kinach [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.