Star Tv

Bill na Melinda Gates wametangaza talaka yao baada ya miaka 27 ya ndoa, wakisema hawaamini tena kama wanaweza kuwa pamoja kama wanandoa.

Wananndoa hao wameeleza kuwa; "Baada ya kufikiria sana na kufanya kazi nyingi juu ya uhusiano wetu, tumefanya uamuzi wa kumaliza ndoa yetu," wawili hao walisema katika ujumbe walioutuma twitter.

Walikutana kwa mara ya kwanza miaka ya 1980 wakati Melinda alipojiunga na kampuni ya Bill ya Microsoft.

Wanandoa hao Mabilionea wana watoto watatu na kwa pamoja wanaendesha Wakfu wa Bill & Melinda Gates.

Shirika hilo limetumia Mabilioni ya pesa kufadhili kampeni mbalimbali ikiwemo magonjwa ya kuambukizana na kuhamasisha chanjo kwa watoto.

Wawili hao pamoja na mwekezaji Warren Buffett wanahusika na mpango wa Ahadi ya kutoa, ambao unawataka mabilionea kujitolea utajiri wao mwingi kwa malengo ya kuwasaidia watu .

Bill Gates ndiye mtu wa nne tajiri zaidi ulimwenguni, kulingana na Forbes, na ana mali ya thamani ya $ 124bn (£ 89bn).

Alipata pesa kupitia kampuni aliyoianzisha miaka ya 1970, Microsoft, kampuni kubwa ya programu ulimwenguni.

Wawili hao walichapisha taarifa hiyo wakitangaza talaka yao kwenye Twitter.

"Katika kipindi cha miaka 27 iliyopita, tumewalea watoto watatu wa ajabu na kujenga wakfu ambao unafanya kazi ulimwenguni kote kuwezesha watu wote kuishi maisha yenye afya, yenye tija," ujumbe huo ulisema

Melinda alijiunga na Microsoft kama msimamizi wa bidhaa mnamo 1987, na hao wawili walikaa pamoja kwenye dhifa ya chakula cha jioni cha biashara mwaka huo huko New York.

Walianza kuchumbiana, lakini kama Bill alivyokiambia kipindi kimoja cha Netflix: "Tulijaliana sana na kulikuwa na uwezekano wa mawili kutokea: ama tungeachana au tungeoana."

Melinda alisema alimpata Bill akiwa mtu wa kawaida inaonekana hata katika maswala ya moyo aliandika orodha kwenye ubao mweupe na "faida na hasara za kuoa".

Walioana mnamo 1994 katika kisiwa cha Lanai cha Hawaii,wakikiripotiwa kukodi helikopta zote za eneo hilo kuwazuia wageni wasiohitajika kupaa na kuja harusini mwao bila kualikwa.

Chanzo:BBCSwahili

Latest News

“TUTAJIRIDHISHA KABLA YA KUKUBALI CHANJO YA CORONA”- Rais Samia.
14 May 2021 18:24 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kupokea chanjo ya virusi vya Corona ni lazi [ ... ]

SOMALIA YATANGAZA KUREJESHA UHUSIANO NA KENYA.
06 May 2021 17:57 - Grace Melleor

Somalia imetangaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo m [ ... ]

KENYA NA TANZANIA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA.
05 May 2021 15:39 - Grace Melleor


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya pamoja na kuondoa vikwazo visivy  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.