Star Tv

Marekani na Uingereza zimechukua juhudi za haraka za kuisaidia India mashine za kupumulia na vifaa vya chanjo, baada ya hali ya taifa hilo kuelezwa na Shirika la Afya Duniani kuwa mbaya zaidi.

Mataifa hayo mawili yamefikia hatua hiyo kwa kuongeza nguvu kwa taifa la India kama juhudi za haraka za kuisaidia India mashine za kupumulia na vifaa vya chanjo.

Hii ni mara baada ya hali ya taifa hilo kuelezwa na Shirika la Afya Duniani kuwa hali ya maambukizi ya virusi vya corona nchini India ni mbaya zaidi, huku Italia ikianza kuondosha vizuizi vya kukabiliana na janga la Covid-19.

India yenye idadi ya watu bilioni 1.3, inapambana na ongezeko kubwa la maambukizi na hospitali zimezidiwa ambapo pia vituo vya kuchoma maiti kama utaratibu wa mazishi ya Kihindi vinafanya kazi hiyo kwa wakati wote.

Kwa rekodi za jana Jumatatu kwa mfano, kumekuwa na maambukizi mapya 352,991 na vifo 2,812 nchini humo.

Kiwango hicho kimetajwa kuwa ni cha juu zaidi kuwahi kutokea tangu kuzuka kwa janga la virusi vya coroa ulimwenguni.

Aidha, Brazil nayo imekuwa tafa lingine linalilozua kuingizwa kwa chanjo ya Urusi, Sputnik V kwa kutoa sababu ya kuhitaji muda wa kujiridhisha kutokana na hofu ya usalama wake.

Latest News

“TUTAJIRIDHISHA KABLA YA KUKUBALI CHANJO YA CORONA”- Rais Samia.
14 May 2021 18:24 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kupokea chanjo ya virusi vya Corona ni lazi [ ... ]

SOMALIA YATANGAZA KUREJESHA UHUSIANO NA KENYA.
06 May 2021 17:57 - Grace Melleor

Somalia imetangaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo m [ ... ]

KENYA NA TANZANIA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA.
05 May 2021 15:39 - Grace Melleor


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya pamoja na kuondoa vikwazo visivy  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.