Star Tv

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeingilia kati sakata la kusambazwa kwa video zisizo na maadili linalomuhusu msanii Harmonize kwa kutoa taarifa inayoeleza kusikitishwa na kitendo hicho kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii.

BASATA wametoa onyo na kukemea vikali vitendo hivyo ambapo imewataka wahusika kuacha tabia hiyo na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa msanii atakayebainika kuendelea kutenda vitu hivyo.

"Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limesikitishwa na matukio na mienendo ya wasanii wa Tanzania kwenye mitandao ya kijamii kwa kushamiri vitendo vya matumizi ya lugha zisizo na staha, malumbano, kukashifiana na usambazaji wa taarifa na video zenye mwelekezo wa kudhalilishana, vitendo hivi ni kinyume na kanuni ya Baraza"-Imeeleza Taarifa ya BASATA.

Taarifa hiyo ya BASATA imeeleza kuwa inatoa onyo kwa Wasanii kuachana na kadhia hiyo; "Baraza linatoa onyo na kukemea vikali mienendo na vitendo hivi na kuwataka wahusika wote kuacha mara moja tabia hiyo, Baraza litachukua hatua kali kwa msanii yeyote atakayebainika kuendelea kutenda vitendo ambavyo ni kinyume na sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya sanaa".

BASATA imesema inategemea kuona hali ya Upendo, Amani, Mshikamano na Ushirikiano vinaendelezwa kama ilivyokuwa awali kwa Wasanii pamoja na Wadau wa Sanaa.

Latest News

“TUTAJIRIDHISHA KABLA YA KUKUBALI CHANJO YA CORONA”- Rais Samia.
14 May 2021 18:24 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kupokea chanjo ya virusi vya Corona ni lazi [ ... ]

SOMALIA YATANGAZA KUREJESHA UHUSIANO NA KENYA.
06 May 2021 17:57 - Grace Melleor

Somalia imetangaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo m [ ... ]

KENYA NA TANZANIA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA.
05 May 2021 15:39 - Grace Melleor


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya pamoja na kuondoa vikwazo visivy  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.