Star Tv

Kituo cha kudhibiti magonjwa nchini Marekani (CDC) kimetoa tahadhari kwa raia wake kutofanya safari nchini Kenya kwa maelezo kuwa nchi hiyo ina kiwango kikubwa cha maambukizi ya COVID-19, kitaalamu (A Level 4 alert).

Tahadhari hiyo imetolewa Aprili 07, ikionya juu ya usalama wa kiafya kutokana na kasi ya maambukizi ya corona nchini Kenya pamoja na ongezeko la uhalifu, ugaidi na utekaji.

Wasafiri wa Marekani wameshauriwa na CDC, kuangalia kurasa ya idara ya usafiri kabla ya kupanga safari yeyote kutokana na changamoto ya COvid 19.

Licha ya tahadhari hiyo kutolewa ndege za kimataifa bado zinafanya kazi nchini Kenya.

Mwishoni mwa mwezi Machi, Rais Uhuru Kenyatta alitangaza zuio la kukutoka nje katika kaunti tano nchini humo ukiwemo mji mkuu Nairobi, Kajiado, Machakos, Kiambu na Nakuru ili kuzuia usambaaji wa virusi vya Corona.

Hatua hii ilikuja kwasababu Kiwango cha maambukizi kimezidi mara kumi zaidi kwa mujibu wa maelezo ya Rais Kenyatta.

 

Latest News

RAIS TSHISEKEDI ADHIBITI BARAZA LAKE JIPYA LA MAWAZIRI.
13 Apr 2021 18:22 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu alitangaza baraza jipya la Mawaziri katika hatua ambayo inaimar [ ... ]

MALIPO YA NDEGE MPYA TATU YAKAMILIKA.
13 Apr 2021 18:04 - Grace Melleor


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema tayari serikali imekamilisha malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu.

WASAFIRI KUTOKA KENYA KUINGIA KARANTINI KWANZA IRELAND.
12 Apr 2021 13:43 - Grace Melleor

Wasafiri wanaoelekea Ireland kutoka Kenya watalazimika kujitenga kwa wiki mbili baada ya kuwasili katika nchi hiyo ya ba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.