Star Tv

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema anafikiria kuunda kamati ya wataalamu watakaoangalia kwa upana wake kitaalamu na kuishauri serikali suala la Ugonjwa wa COVI-19 ili kupata mustakabali wa kukabiliana na ugonjwa huo.

Rais Samia ametoa kauli hiyo wakati akiwaapisha Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali na Taasisi tofauti katika ikulu ya Jijini Dar es Salaam.

"Nakusudia niunde kamati ya wataalamu, waangalie suala la Covid -19, kwa upana wake alafu watushauri serikali…. Halifai kulinyamazia bila kufanya tafiti ya kitaalamu.”-Rais Samia Suluhu Hassan.

Rai Samia amesisitiza kuwa kamati hiyo itashauri nini kifanyike ili kupambana na gonjwa hili linaloitikisa dunia tangu mwaka 2019.

“Watuambie upeo wa suala hili...Hatuwezi kujitenga kama kisiwa na hatuwezi kupokea yanyoletwa bila kufanya cha kwetu, Rais Kikwete alituambia akili za kuambiwa changanya na zako, tuweke na zetu tuwe na msimamo maalum unaoeleweka, sio tunasoma tu mambo ya Covid 19 Ulimwenguni, Tanzania deshi...deshi…. deshi haieleweki, tueleweke kama tunakubali au tunakataa”-Ameeleza Rais Samia.

Katika Upande mwingine Rais ameitaka Wizara ya Habari, Sanaa na Utamaduni kuvifungulia vyombo vyote vya habari vilivyokuwa vimefungiwa na kusisitiza kuwa vyombo hivyo vifuate kanuni na taratibu zilizowekwa.

“Wizara ya Habari, nasikia kuna Vyombo vya Habari mmevifungia fungia, sijui Viji- TV vya mikononi (Online Tv) vile, vifungulieni lakini wafuate sheria na miongozo ya Serikali, tusiwape mdomo wa kusema tunabinya Uhuru wa Vyombo vya Habari, tusifungie tu kibabe”-Rais Samia.

Aidha Rais Samia amewasisitiza viongozi wote walioapishwa leo kwenda kutimiza majukumu yao ipasavyo”

“Tumezoea tunapokwenda kwenye ziara Mikoani na Wilayani, tunapokewa na mabango ya Wananchi wakilalalimikia kero mbalimbali na mabango yale sio mambo ya kushughulikiwa ngazi za juu, naomba tunapokuja tukikuta bango iwe mambo ya Kitaifa, tukikuta bango moja aidha Mkurugenzi au Mkuu wa Wilaya umekwenda...hii haina maana mkazuie Watu kuandika kero zao, kero za Wananchi mkashughulikie na tukikuta malalamiko kwamba mnawafinya wasiseme tutawashughulikia”-Amebainisha Rais Samia.

Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara, pamoja na Wakuu wa Mashirika walioteuliwa April 04, wameapishwa leo Aprili 06 mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika Ikulu ya Magogoni Jijini Dar es Salaam.

 

Latest News

“TUTAJIRIDHISHA KABLA YA KUKUBALI CHANJO YA CORONA”- Rais Samia.
14 May 2021 18:24 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kupokea chanjo ya virusi vya Corona ni lazi [ ... ]

SOMALIA YATANGAZA KUREJESHA UHUSIANO NA KENYA.
06 May 2021 17:57 - Grace Melleor

Somalia imetangaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo m [ ... ]

KENYA NA TANZANIA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA.
05 May 2021 15:39 - Grace Melleor


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya pamoja na kuondoa vikwazo visivy  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.