Star Tv

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu wa wizara na wakuu wa taasisi walioapishwa leo kuelewa majukumu yao na kujipanga kuwatumikia Watanzania.

Akizungumza mara baada ya viongozi hao kuapa mbele ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu amewataka makatibu Wakuu wote walioapishwa leo Aprili 6,2021 kuwa na nidhamu pamoja na kuwatumikia ipasavyo Watanzania.

"Wote mlioapishwa leo mkahakikishe mnakuwa na mpango kazi madhubuti, mnakuwa na nidhamu ya hali ya juu pamoja na kuhakikisha mnasimamia ukusanyaji wa maduhuli ili kusongesha vyema maendeleo ya nchi yetu"-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Amesema ni lazima wasimame kwenye nafasi zao kuhakikisha uchumi unakua kwa kiwango kilichopangwa.

“Nendeni mkasome na kuelewa wizara zenu na majukumu yake na mkafanye kazi kwa ajili ya kwatumikia Watanzania ipasavyo, jukumu lenu kubwa ni kuhakikisha shughuli za kila siku za wizara zinakwenda vizuri, muwe na mpango kazi utakaokidhi matakwa ya watanzania,” – Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Aidha, Waziri mkuu Majaliwa amesema tayari nchi imefanikiwa kuingia katika kundi la nchi zenye uchumi kati, hivyo hatua iliyobaki ni kufikisha maendeleo kwa mwananchi mmoja mmoja, suala ambalo viongozi wote wanapaswa kulipa kipaumbele.

Latest News

RAIS TSHISEKEDI ADHIBITI BARAZA LAKE JIPYA LA MAWAZIRI.
13 Apr 2021 18:22 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu alitangaza baraza jipya la Mawaziri katika hatua ambayo inaimar [ ... ]

MALIPO YA NDEGE MPYA TATU YAKAMILIKA.
13 Apr 2021 18:04 - Grace Melleor


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema tayari serikali imekamilisha malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu.

WASAFIRI KUTOKA KENYA KUINGIA KARANTINI KWANZA IRELAND.
12 Apr 2021 13:43 - Grace Melleor

Wasafiri wanaoelekea Ireland kutoka Kenya watalazimika kujitenga kwa wiki mbili baada ya kuwasili katika nchi hiyo ya ba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.