Star Tv

Mtu mmoja amepigwa risasi na kufariki baada ya kuliendesha gari lake kuelekea kwa maafisa wawili wa polisi karibu na majengo ya bunge nchini Marekani, Ambaye pia amesababisha kifo cha Afisa wa polisi mmoja.

Maafisa wa polisi wamesema gari hilo lililokuwa likiendeshwa kuelekea walipo maafisa wa polisi liligonga vizuizi vya usalama, kisha mshukiwa aliyekuwa akiliendesha akatoka nje akiwa amebeba kisu mkononi na kukimbia kuelekea kwa maafisa wa polisi.

Aidha, imeelezwa kuwa fisa mmoja wa polisi amekufa kufuatia kisa hicho.

Mtuhumiwa wa shambulizi hilo inaelezwa kuwa, aliliendesha gari kuelekea kwa maafisa hao wawili waliokuwa wakishika doria katika majengo ya bunge ya Marekani mjini Washington DC, kabla ya kupigwa risasi na maafisa wa polisi.

Mshukiwa huyo alikaidi amri kutoka kwa maafisa wa usalama na ndipo alipopigwa risasi, na katika harakati za kumpeleka kupata matibabu baadaye alifariki akiwa hospitalini.

Rais wa Marekani Joe Biden ambaye hayuko mjini Washington kwa sasa amesema yeye pamoja na mke wake Jill Biden wamesikitishwa na shambulizi hilo.

"Jill pamoja na mimi tulisikitishwa kusikia kuhusu shambulizi katika eneo la kizuizi cha usalama kwenye majengo ya bunge ambalo limesababisha kifo cha afisa wa polisi William Evans wa kikosi cha polisi cha Capitol."Tunatuma salamu za rambirambi kwa familia ya Evans na yeyote anayehuzunika kufuatia kifo chake."- Biden amesema kwenye taarifa.

Maeneo hayo ya majengo ya bunge yamefungwa na usalama kuimarishwa, Ambapo kwasasa Maafisa wa usalama wamesema wameanzisha uchunguzi dhidi ya kisa hicho.

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.