Star Tv

Hii ni mara baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kumpendekeza Philip Isdory Mpango kuwa Makamu wake wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jina hilo la Dkt. Philip Mpango liliwasilishwa bungeni asubuhi ya Jumanne Machi 30,2021 na mpambe wa rais katika bahasha maalum.

Aidha, Baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kupokea jina lake alilitangazia bunge jina hilo lililopendekezwa na Rais Samia.

Bunge la Tanzania limempigia kura ili kuthibitisha uteuzi huo wa Dkt. Mpango, Ambapo baada ya kura hizo kupigwa na Wabunge ameshinda kwa kura 363 ambazo zilipigwa kama kura za ndio kutoka kwa Wabunge waliokuwepo Bungeni.

Wakati Spika wa Bunge Job Ndugai akitangaza matokeo hayo amebainisha kuwa; "Katika kura zilizopigwa kwa Dkt. Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais hakuna kura zilizoharibika, hivyo Bunge limethibitisha Dkt. Philip Mpango kuwa ndiye Makamu wa Rais wa Tanzania Mteule ambaye ataapishwa tarehe na muda utakaopangwa".

Dkt. Mpango amekuwa waziri mwandamizi katika serikali ya hayati John Magufuli akihudumu kama waziri wa fedha.

Kabla ya jina hilo kuwasilishwa bungeni hii leo, kwanza liliwasilishwa katika Kamati kuu ya chama tawala CCM na kuthibitishwa.

Kwa mujibu wa Katiba inabainisha kuwa asilimia 50 ya Wabunge wanatakiwa kuukubali uteuzi wa Makamu wa Rais ili kuthibitisha.

Dkt. Philip Mpango amekuwa Waziri wa Fedha na Mipango katika Serikali ya Awamu ya Tano, ambaye aliteuliwa katika Baraza la mwanzo la Mawaziri la Rais John Magufuli.

Dkt. Mpango ni mchumi mwenye shahada ya uzamivu ya uchumi, Amewahi kuwa Mchumi Mwandamizi Benki ya Dunia, Mkuu wa Kamati ya kumshauri Rais Jakaya Kikwete wakati huo kuhusu masuala ya uchumi, Katibu binafsi wa Rais anayeshughulikia masuala ya uchumi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi.

Latest News

ZUMA ATAKIWA KUCHAGUA ADHABU KWA KUDHARAU MAHAKAMA.
14 Apr 2021 17:55 - Grace Melleor

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ametakiwa mpaka kufikia Jumatano awe amependekeza adhabu ambayo mahakama kuu  [ ... ]

RAIS TSHISEKEDI ADHIBITI BARAZA LAKE JIPYA LA MAWAZIRI.
13 Apr 2021 18:22 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu alitangaza baraza jipya la Mawaziri katika hatua ambayo inaimar [ ... ]

MALIPO YA NDEGE MPYA TATU YAKAMILIKA.
13 Apr 2021 18:04 - Grace Melleor


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema tayari serikali imekamilisha malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.