Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza siku 14 za maombolezo pamoja na bendera kupepea nusu mlingoti kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Maguful kilichotokea Machi 17,2021.
Makamu wa Rais ametangaza msiba huo kupitia Televisheni ya Taifa (TBC) ambapo amesema kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefariki Dunia kutokana na maradhi ya moyo.
"Rais alilazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Machi 06, akaruhusiwa Machi 07. Kabla ya kupelekwa Hospitali ya Mzena Machi 14,2021".-Alisema Makamu wa Rais.
Kufuatia msiba huu wa taifa, Makamu wa Rais ametangaza siku 14 za maombolezo ambapo pia amesema bendera zitapepea nusu mlingoti.
Marehemu Rais Magufuli alizaliwa Oktoba 29,1959, Alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2015 na amefarika Machi 17, 2021 katika hatamu ya awamu ya pili ya urais wake.
#RIPRaisJohnPombeMagufuli