Star Tv

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Ripoti zinasema Seif Bamporiki aliuawa alipokuwa akiwasilisha samani kwa mteja Jumapili mchana mjini Cape Town.

Haijabainika kama kifo chake kilichochewa kisiasa.

Aidha, Waliomvamia walichukua simu zake za rununu na waleti kabla ya kutoroka eneo la tukio, na hakuna aliyekamatwa kuhusiana na kisa hicho.

Bw. Bamporiki alikuwa mshirikishi wa chama cha Rwanda National Congress.

Msemaji wa chama hicho, Etienne Mutabazi ameiambia BBC kwamba mteja alikuwa amewasiliana na Bw. Bamporiki ambaye anaendesha duka la kuuza vitanda,  kuuliza kama ana kitanda cha kuuza.

"Mteja kisha aliomba kitanda hicho kupelekwa katika mji wa Nyanga na kuamua kutumia gari na Bwana Bamporiki na mwenzake kwenda eneo ambalo kitanda kilitakiwa kupelekwa"-Mutabazi.

Maelezo ya kile kilichotokea baada ya hapo bado hayajathibitishwa, lakini Bw. Bamporiki aliuawa kwa risasi moja ambayo ilipigwa kupitia dirisha la gari.

Mji wa Nyanga unafahamika kuwa moja ya miji hatari nchini Afrika Kusini, Ambapo wakati mmoja mji huo ulikuwa na idadi ya juu zaidi ya mauji kwa mwaka.

Latest News

“MAISHA HAYAJI MARA MBILI, TUSIPOTOSHE KUHUSU CHANJO”-IGP. Simon Sirro.
29 Jul 2021 11:30 - Grace Melleor

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP. Simon Sirro, amewataka Wananchi na Watanzania kwa ujumla wasidanganywe na watu wacha [ ... ]

“MIMI NI MAMA, BIBI, MKE NA RAIS, SIWEZI KUJIWEKA KATIKA HATARI”-Rais Samia....
28 Jul 2021 10:26 - Grace Melleor

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokea chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19, Ambayo ameizindua leo Julai 28, Katik [ ... ]

MSICHANA AUAWA KWA KUVAA JEANS.
28 Jul 2021 09:51 - Grace Melleor

Msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Neha Paswan, mwenye umri wa miaka 17, anadaiwa kupigwa hadi kufa na watu wa fam [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.