Star Tv

Mamia ya wazanzibari wanaendelea kumiminika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja vilivyopo mjini Ujunga ambapo ndipo mwili wa aliyekuwa makamo wa kwanza wa Urais Zanzibar utakapopelekwa kwa ajili ya dua kabla ya kusafirishwa kijijini kwake Mtambwe, kisiwani Pemba.

Kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad kinaonekana kuleta simanzi kubwa kwa wakazi wa visiwani humo na watanzania kwa ujumla.

Kisiwani Pemba ambapo ndio alikuwa ngome yake Kuu wakati wa uhai wake, punde tu baada ya taarifa za kifo chake kuenea, baadhi ya maduka yamefungwa na shughuli nyingi za mji kusimama, hivyo kufanya mji huo kuzizima kwa saa kadhaa.

Ratiba ya mazishi inaonyesha kuwa, baada ya mwili wa marehemu utaswaliwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja na hatimaye kwenda kupumzishwa huko kijijini kwao Mtambwe.

Wakati maombolezo yakiendelea, wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu wameonekana wakiwanyunyizia watu sanitaiza huku wachache Wakionekana kuchukua tahadhari ya kuvaa barakoa.

Mpaka kifo chake, Maalim alikuwa makamo wa kwanza wa urais Zanzibar chini ya serikali ya umoja wa kitaifa.

Maalim anazikwa wakati watanzania wapo katika kuomboleza msiba mwengine wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi aliyefariki jana Februari 17, majira ya saa tatu usiku.

Chanzo na BBC Swahili.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.