Star Tv

Polisi Mjini New York wameeleza kuwa Baba wa mwanamuziki wa miondoko ya kufokafoka, Nicki Minaj, 64, ameaga dunia baada ya kugongwa na gari kisha dereva kukimbia mjini New York.

Robert Miraj alikuwa akitembea kandokando ya barabara katika kisiwa cha Long siku ya Ijumaa na kugongwa na gari, kisha dereva wa gari hiyo aliendelea na safari, polisi katika kaunti ya Nassau imesema.

Miraj alipelekwa hospitalini ambako alithibitishwa kufariki siku ya Jumamosi.

Polisi wametaka shuhuda yeyote wa tukio hilo baya kujitokeza. Gazeti la the Guardian limeripoti .

Minaj, 38, kwa jina la Onika Tanya Miraj alizaliwa huko Trinidad na alikulia jijini New York City borough of Queens.

Aidha, Mwanamuziki huyo hajajitokeza kuzungumza chochote kuhusu kifo cha baba yake.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.