Star Tv

Bunge la uwakilishi nchini Marekani limepiga kura ya kutokuwa na imani dhidi ya rais Donald Trump kwa kuchochea ghasia zilizosababisha uvamizi wa jumba la bunge la Capitol.

Wabunge 10 wa chama cha Republican walishirikiana na wenzao wa chama cha Democrat kupitisha kura hiyo ya kumshtaki rais kwa 232 dhidi ya wabunge 197 waliopinga hatua hiyo.

Ni rais wa kwanza katika historia ya Marekani kupigiwa kura ya kutokuwa na imani mara mbili ama kushtakiwa kwa makosa ya uhalifu na bunge hilo la Congress.

Rais Trump ambaye ni mwanachama wa Republican sasa atakabiliwa na kesi katika bunge la seneti ambapo iwapo atapatikana na hatia huenda akapigwa marufuku kushikilia wadhfa wowote wa ofisi ya umma.

Bwana Trump anaachia madaraka tarehe 20 mwezi Januari kufuatia kushindwa kwake katika uchaguzi mkuu mwezi Novemba uliomtangaza Joe Biden mshindi.

Bunge hilo linalodhibitiwa na wabunge wengi wa Democrat lilipiga kura siku ya Jumatano saa kadhaa baada ya mjadala mkali huku walinzi wa kitaifa wakiimarisha usalama ndani na nje ya jumba la bunge hilo.

Shirika la kijasusi nchini Marekani FBI limeonya kwamba kuna uwezekano wa kuzuka kwa maandamano katika majimbo yote 50 kabla ya kuapishwa kwa rais mteule Joe Biden wiki ijayo.

Katika kanda ya video iliotolewa baada ya kura hiyo kupigwa , bwana Trump aliwataka wafuasi wake kusalia watulivu lakini hakuzungumzia kwamba alikuwa amepigiwa kura ya kutokuwa na imani naye bungeni.

Ghasia na uharibifu hauna nafasi katika taifa letu…hakuna mfuasi wangu ambaye angependelea kufanyika kwa ghasia za kisiasa' , alisema akionesha huzuni na mwenye kutaka maridhiano.

Rais huyo alituhumiwa na bunge la Congress kwa kuchochea ghasia ziizosababisha uvamizi wa Jumba la bunge la Capitol kufuatia hotuba yake aliyotoa tarehe sita mwezi Januari katika mkutano wa hadhara nje ya Ikulu ya Whitehouse.

Aliwataka wafuasi wake kuandamana kwa amani na uzalendo ili sauti zao zisikike, lakini pia kukabiliana na uchaguzi ambao alidai kwamba ulikumbwa na udanganyifu mkubwa.

Kufuatia matamshi hayo ya rais Trump, wafuasi wake walivunja na kuingia katika Jumba la Capitol , na kuwalazimu wabunge kuahirisha kikao cha kuidhinisha ushindi wa rais mteule Joe Biden na baadaye kujificha.

Jumba hilo lilifungwa kwa muda na watu watano wakafariki wakati wa ghasia hizo.

Latest News

RAIS JOE BIDEN AMUONYA RAIS WA URUSI VLADMIR PUTIN
27 Jan 2021 06:39 - Grace Melleor

Rais wa Marekani Joe Biden amemuonya kiongozi wa Urusi Vladimir Putin kuhusu kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo.

WANASHERIA WA BOBI WINE WARUHUSIWA KUMUONA MTEJA WAO.
22 Jan 2021 08:40 - Grace Melleor

Jeshi la UPDF na polisi nchini Uganda wamewaruhusu wanasheria wa waliokuwa wa mgombea wa kiti cha urais Robert Kyagulany [ ... ]

UINGEREZA YAPIGA MARUFUKU ABIRIA KUTOKA TANZANIA, DRC.
22 Jan 2021 08:18 - Grace Melleor

Abiria wote kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo hawataruhusiwa kuingia nchini Uingereza na katika matai [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.