Raia wa Uganda hii leo Januari 14,2021 wanapiga kura kumchagua rais na wawakilishi wapya wa bunge.
Akizungumza siku ya Jumatano mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo jaji Simon Byabakama aliserma kwamba wapiga kura wa kiume ni zaidi ya milioni tisa huku wenzao wa jinsia ya kike wakiwa zaidi ya milioni tisa.
Katika uchaguzi huo rais Yoweri Museveni ambaye anatetea wadhfa wake anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mwanamuziki wa zamani maarufu Bobi Wine.
Bobi Wine ni mgombea ambaye amevutia idadi kubwa ya vijana nchini humo.
Rais Museveni anagombea muhula wa sita baada ya kuwa madarakani kwa miaka 35.
Hata hivyo rais Museveni anajivunia utawala wake wa muda mrefu ambapo amefanya baadhi ya maenedeleo.
Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, anasema kuwa anawakilisha kizazi kipya cha vijana wa nchini humo, huku Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 76, akisema kuwa anasimamia ustawi.
Chanzo na BBC Swahili.