Star Tv

Taifa la Malawi limepata pigo kubwa baada ya mawaziri wake wawili kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa COVID 19.

Waziri wa habari wa Malawi, Gospel Kazako amethibitisha kuwa mawaziri hao ambao ni Waziri wa serikali za mitaa, Lingson Belekanyama na Waziri wa uchukuzi Sidik Mia wamefariki ndani ya masaa mawili tofauti.

Mwishoni mwa juma, rais wa nchi hiyo Lazarus Chakwera alitoa hotuba maalumu kwa njia ya radio kwa taifa akitoa wito wa kuheshimiwa kwa hatua zilizowekwa za kupambana na maambukizi ya Covid 19 kufuatia ongezeko kubwa katika vifo na maambukizi ya virusi hivyo.

Bwana Chakwera anatarajiwa kutoa hotuba nyingine kwa taifa kwa mujibu wa Kazako.

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.