Star Tv

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis amesema matumizi ya chanjo zilizotengenezwa kutokana na seli za mimba zilizotolewa "unakubalika kimaadili".

Licha ya tamko hilo kutolewa na Vatican, lakini Kanisa hilo limesisitiza kwamba, hatua hiyo haimaanishi "inaaunga mkono rasmi" utoaji mimba uliofanyika.

Kusipokuwa na njia nyingine mbadala, chanjo kama hizo "zinaweza kutumiwa kwa dhamira njema",Vatican imesema.

Kwa mujibu wa Wataalamu wa Afya, Chanjo kadhaa zimetengezwa kwa kutumia vijusi vya mimba iliyotolewa miongo kadhaa iliyopita, Hata hivyo hakuna hata chanjo moja zilizotengezwa zina na seli za vijusi.

"Chanjo zote zimeidhinishwa kuwa salama na zinaweza kutumiwa kwa nia njema na ufahamike kwamba matumizi ya chanjo kama hizi sio ushirikiano rasmi na utoaji mimba ambao seli zinazotumiwa katika utengenezaji wa chanjo zinatokana,"-Usharika wa Vatican wa Mafundisho ya Imani ulitangaza katika taarifa Jumatatu.

Taarifa hiyo iliyoidhinishwa na Papa Francis, pia ilisema "sharti la kimaadili" ni kuhakikisha nchi masikini zinapata chanjo inayofanya kazi vyema.

Suala la kukubali au kupinga chanjo ya corona limewagawanya viongozi wa kidini, wakati kangamano la Marekani la Makasisi wa Katoliki wiki iliyopita likionekana kuliunga mkono.

 

 

Latest News

RAIS JOE BIDEN AMUONYA RAIS WA URUSI VLADMIR PUTIN
27 Jan 2021 06:39 - Grace Melleor

Rais wa Marekani Joe Biden amemuonya kiongozi wa Urusi Vladimir Putin kuhusu kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo.

WANASHERIA WA BOBI WINE WARUHUSIWA KUMUONA MTEJA WAO.
22 Jan 2021 08:40 - Grace Melleor

Jeshi la UPDF na polisi nchini Uganda wamewaruhusu wanasheria wa waliokuwa wa mgombea wa kiti cha urais Robert Kyagulany [ ... ]

UINGEREZA YAPIGA MARUFUKU ABIRIA KUTOKA TANZANIA, DRC.
22 Jan 2021 08:18 - Grace Melleor

Abiria wote kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo hawataruhusiwa kuingia nchini Uingereza na katika matai [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.