Star Tv

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema kuwa bado hajaona mtu mwenye uwezo wa kuiongoza Uganda kwa sasa, hivyo ataendelea kuwa madarakani.

Museveni mwenye umri wa miaka 76, ameliongoza taifa la Uganda kwa zaidi ya miongo mitatu.

Akizungumza na viongozi wa chama chake cha National Resistance Movement (NRM) hapo jana, amesema kwamba wapinzani wake hawana vigezo vya kuliongoza taifa la Uganda.

"Ninakasirika sana ninaposikia watu wakiniambia niondoke madarakani,”-Museveni alinukuliwa na vyombo vya habari nchini humo.

Na kuongeza kuwa;“ Wapiga kura ndio wanaoamua, hata nikiondoka nani ataweza kuliongoza taifa hili, nitaondoka tu iwapo kuna mtu wa maana nitakayeona naweza kumuachia Uganda".

Rais Museveni ambaye aliingia madarakani kwa njia ya mapigano ya msituni amekaa madarakani tangu mwaka 1986.

Katika uchaguzi mkuu wa Uganda unaotarajiwa kufanyika Januari 14 mwakani una wagombea 11 wa nafasi ya Urais, 10 kati yao wakitaka kuchukua nafasi ya Yoweri Museveni wa chama tawala cha NRM anayetaka kutetea nafasi yake kwa muhula wa sita.

Latest News

RAIS JOE BIDEN AMUONYA RAIS WA URUSI VLADMIR PUTIN
27 Jan 2021 06:39 - Grace Melleor

Rais wa Marekani Joe Biden amemuonya kiongozi wa Urusi Vladimir Putin kuhusu kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo.

WANASHERIA WA BOBI WINE WARUHUSIWA KUMUONA MTEJA WAO.
22 Jan 2021 08:40 - Grace Melleor

Jeshi la UPDF na polisi nchini Uganda wamewaruhusu wanasheria wa waliokuwa wa mgombea wa kiti cha urais Robert Kyagulany [ ... ]

UINGEREZA YAPIGA MARUFUKU ABIRIA KUTOKA TANZANIA, DRC.
22 Jan 2021 08:18 - Grace Melleor

Abiria wote kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo hawataruhusiwa kuingia nchini Uingereza na katika matai [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.