Star Tv

Wabunge 19 wa viti maalum waliovuliwa uanachama wa chama cha upinzani Chadema, wamesema wataendelea kuwa 'wanachama wa hiyari' wa chama hicho huku wakipanga kukata rufaa juu ya adhabu waliyopewa.

Viongozi hao 19 hii leo Disemba Mosi wakiongozwa na Halima Mdee wamesema kuwa baada ya kuvuliwa uanachama na Kamati Kuu, sasa wataenda ngazi ya juu kimaamuzi ya Halmashauri Kuu, ili kukata rufaa.

Hayo yamejiri leo wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo pia Mdee hakujibu maswali ya waandishi hao yakuwa ni nani aliyepeleka majina yao Tume ya Uchaguzi ya (NEC) na nani aliyewapa idhini ya kula kiapo cha ubunge.

"Siwezi kujibu hapa juu ya hoja hizo mbili kuhusu mchakato wa kupatikana kwetu. Hoja hizo ndiyo msingi wa rufaa yetu, hivyo siwezi kujadili kesi yetu na vyombo vya habari kabla hatujaipeeka katika mamlaka husika, Baraza Kuu”-Halima Mdee.

Kwa mujibu wa uongozi wa Chadema, Katibu Mkuu wa chama John Mnyika hakuwasilisha majina ya wateule wa viti maalum NEC, na hawakutoa idhini ya kada yoyote kuapa Bungeni.

Aidha, kuhusu suala la kutohudhuria kwenye kikao cha kamati kuu amesema kuwa, hawakutokea katika kikao kilichochukua uamuzi dhidi yao kwa kuwa walihofia usalama wao pamoja na kujiepusha na maamuzi ya jazba.

"Kulikuwa na uhamasishaji wa hali ya juu mitandaoni uliofanywa na baadhi ya viongozi wa juu wakitaka wanachama wajitokeze ili kutushughulikia... Pili, pande zote mbili kulikuwa na hasira, tuliamini maamuzi yangefikiwa kwa jazba...tuliomba kuahirishwa kwa kikao cha Kamati Kuu kwa wiki moja lakini tukakataliwa. Hivyo, tuliona nio busara zaidi kutokuhudhuria"-ameeleza Mdee.

Itakumbukwa kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kilipata mbunge mmoja wa jimbo la Nkasi katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, hata hivyo kutokana na nafasi ya mbunge huyo mmoja, chama hicho kwa mujibu wa katiba kilikidhi vigezo vya kuteua wabunge 19 wa viti maalum.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.