Star Tv

Korea Kaskazini imetahadharisha raia wake kusalia majumbani kutokana na hofu ya ''vumbi la njano'' linalopepea kutoka China kuwa linaweza kubeba virusi vya corona.

Mitaa ya mji mkuu Pyongyang iliripotiwa kuwa mitupu siku ya Alhamisi baada ya tahadhari hiyo kutolewa.

Nchi hiyo ambayo imedai kuwa haina maambukizi ya virusi lakini imekuwa kwenye tahadhari kubwa tangu mwezi Januari, huku ikifunga kabisa mipaka na kuzuia mizunguko ya watu.

Televisheni inayodhibitiwa na serikali ya Korea (KCTV) ilitangaza kipengele cha taarifa ya hali ya hewa siku ya Jumatano , ikitahadharisha kuingia kwa vumbi la njano siku inayofuata.

Vumbi la manjano linahusu mchanga kutoka jangwa la Mongolia na China ambalo hupiga Korea ya Kaskazini na Kusini wakati fulani wa mwaka.

Ubalozi wa Urusi huko Pyongyang umesema katika ukurasa wake wa Facebook kuwa wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini imeionya pamoja na ofisi nyingine za kidiplomasia na mashirika ya kimataifa nchini humo kuhusu dhoruba ya vumbi ikiwataka wageni wote kubaki nyumbani na kufunga madirisha yao vizuri.

Vyombo vya habari nchi jirani ya Korea Kusini pia vimepinga mawazo hayo na kusema haiwezekani kuwa vumbi la manjano kutoka China linaweza kusambaza ugaonjwa wa Covid-19 kuelekea Korea Kaskazini.

Licha ya kudai kuwa nchi hiyo haina maambukizi ya ugonjwa wa corona, kuna hofu kubwa huko Korea Kaskazini na kiongozi Kim Jong-Un amekuwa akifanya mikutano ya hali ya juu kuhakikisha masharti makali yanatekelezwa.

Latest News

RAIS WA CHAD, IDRISS DEBY ATIMIZA MIAKA 30 MADARAKANI.
01 Dec 2020 14:48 - Grace Melleor

Desemba 1, 1990, Idriss Déby alichukua hatamu ya uongozi wa nchi ya Chad kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa, H [ ... ]

“HATUONDOKI CHADEMA, TUNAKATA RUFAA”- Halima Mdee.
01 Dec 2020 13:01 - Grace Melleor

Wabunge 19 wa viti maalum waliovuliwa uanachama wa chama cha upinzani Chadema, wamesema wataendelea kuwa 'wanachama wa h [ ... ]

MTANZANIA ALIYETEKELEZA SHAMBULIZI CHUO CHA GARISSA AJINYONGA GEREZANI.
30 Nov 2020 10:05 - Grace Melleor

Mtanzania Rashid Charles Mberesero aliyehukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2019 baada ya kupatikana na hatia ya kushiriki [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.