Star Tv

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepokea taarifa ya vifo vya watu kumi na mbili vilivyotokana na athari ya mvua inayoendelea kunyesha Jijini Dar es salaam.

Mnamo Oktoba 13, 2020 kuanzia majira ya saa kumi alfajiri katika maeneo mbali mbali ya Jiji la Dar es Salaam, mvua kubwa ilianza kunyesha na kuendelea kunyesha mchana kutwa na kusababisha vifo vya watu 12.

Vifo hivyo vilivyosababishwa na athari za mvua vilitokea katika Mikoa ya Kipolisi Ilala na Kinondoni.

MKOA WA KIPOLISI ILALA.
Jumla watu 8 walifariki dunia baada ya kusombwa na maji.
Mnamo Oktoba 13, 2020 majira ya saa moja jioni mwanamke mmoja aliyefahamika kwa majina ya Mariam Yahaya (45), Mkazi wa Vingunguti, alifariki dunia baada ya kusombwa na maji wakati akijaribu kuokoa vyombo vyake vilivyokuwa vinasombwa na maji, mwili wake ulikutwa unaelea kando ya mto Msimbazi na mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Aidha, miili ya watu watano ilipatikana katika bonde la mto Msimbazi eneo la Jangwani, kati ya hao watu wawili walifahamika kwa majina kama ifuatavyo;
Herieth Kanuti(18), Mwanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari Lutihinda.
Ipyana Mwakifuna(19) Mkazi wa Jangwani, Askari Jeshi la akiba la Mgambo, Huku miili mingine ya watu watatu bado haijatambuliwa ikiwa ni wanaume wawili na mwanamke mmoja.

Tukio lingine la kifo limeripotiwa Oktoba, 14,2020 majira ya saa kumi na mbili na dakika arobaini na tano asubuhi huko Tabata, mwili wa mtu mmoja mwanaume aliyefahamika kwa majina ya Philipo Feliciani(30), Mkazi wa Tabata Kimanga, ulionekana ukiwa umenasa kwenye matope katika mto Tenge, ambaye alifariki dunia Oktoba 13,2020 majira ya saa kumi na mbili jioni baada ya kudondoka na kusombwa na maji alipojaribu kuvuka kwenye kidaraja cha waenda kwa miguu kilichopo Tabata Kimanga na mwili wa mtu mmoja mwingine mwanaume asiyefahamika anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30-35 alikutwa akiwa amefariki dunia katika eneo la Ukonga sabasaba mji mpya.

MKOA WA KIPOLISI KINONDONI.
Jumla ya watoto wawili wa familia moja na watu wazima wawili walifariki dunia kutokana na athari za mvua ambao ni:-
1. Ibrahim Hassani(24),Mkazi wa Kigogo Buyuni,
2. Hussein Awadhi (5) Mkazi wa Kigogo Buyuni na
3. Bakari Awadhi (14), Mkazi wa Kigogo Buyuni.

Watoto hao walifariki dunia kwa kusombwa na maji baada ya nyumba yao iliyopo katika bonde la Kigogo kujaa maji na watoto hao kushindwa kujiokoa na marehemu Ibrahim Hassani alijaribu kumuokoa mtoto mmoja lakini na yeye akasombwa na maji na kufariki dunia.
Pia mnamo tarehe 14 Oktoba, 2020 majira ya saa mbili asubuhi huko Mabibo mwili wa mtu mmoja mwanaume asiyefahamika anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30-35 ulionekana unaelea kwenye mfereji unaopeleka maji katika mto Msimbazi, na miili ya marehemu imehifadhiwa hospitali ya Taifa Muhimbili.

Aidha, Taarifa ya Kamanda Mambosasa imebainisha pia watu watano wa familia moja walifarika dunia kwa ajali ya moto jijini Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linasikitika kuthibitisha kutokea kwa ajali ya Moto na kusababisha vifo vya watu watano wa familia moja.

Mnamo tarehe 13/10/2020 majira ya saa nne kamili usiku huko maeneo ya Pugu nyumba yenye vyumba vinne inayomilikiwa na Edward Katema (37),Mfanyabiashara , Mkazi wa Pugu ,iliteketea kwa moto na kusababisha vifo vya watu wa familia moja ambao ni :-
1. Jackline Frank (27),Mwanafunzi wa Pugu Sekondari.
2. Esther Jeremiah Katemi(15),Mwanafunzi wa Pugu Sekondari.
3. Edward Katemi (11),Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Pugu.
4. Edson Edward Katemi(10) ,Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Green Hill.
5. Ivon Edward Katemi, mtoto wa miaka 4.
Chanzo cha moto ni hitilafu ya umeme iliyoanzia kwenye main switch na miili ya marehemu imeifadhiwa hospitali ya Taifa Muhimbili.

Imetolewa na ;
LAZARO B. MAMBOSASA– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.