Star Tv

Rais anaye maliza muda wake nchini Marekani na mgombea urais kwa awamu nyingine wa chama cha Republican, Donald Trump amesema hataki kushiriki mdahalo na Joe Biden.

Rais Trump amesema haoni haja ya kushiriki mdahalo huo kwa njia ya televisheni kama ilivyokuwa awali ikiwa ni sehemu ya kampeni ya uchaguzi wa urais nchini Marekani, Na ndivyo inavyopendekezwa na kamati ya mdahalo kwa wagombea urais.

Mdahalo huu ungefanyika mbele ya umati wa watu, ambao wangeliuliza maswali kwa wagombea wote, chini ya usimamizi wa Steve Scully katika eneo moja huko Florida.

Aidha, katika mjadala huo baina ya wagombea urais hao wawili Donald Trump pamoja na Joe Biden wangewajibu maswali ambayo wangeulizwa.

Kulingana na muundo huu wa pande mbili, mdahalo wa pili miongoni mwa mitatu kati ya wawili hao, Oktoba 15, ni kwa ajili ya uchaguzi wa urais wa Novemba 3 nchini Marekani, Ambapo ulitarajiwa kufanyika wakati wawili hao wakiwa wamekaa kila mmoja mbali na mwengine, kama tahadhari ya kiafya, wakati rais aliambukizwa virusi vya Corona.

Trump amekiambia kituo cha Fox Business Network wakati alipohojiwa kwa njia ya simu kuwa; "Sitafanya mdahalo kama huo, sitapoteza wakati wangu na mdahalo kama huo, hiyo sio kile ninachokiita mdahalo, amekiambia kituo hicho kwa njia ya simu. Tunatakiwa kuketi nyuma ya kompyuta na kila moja kutoa sera zake na kujibu maswali”.

Timu yake ya kampeni imeongeza kuwa angefanya mkutano wa kampeni badala ya kushiriki kwenye televisheni ana kwa ana.

Kwa upande wake, Joe Biden amebaini kwamba atafuata sheria zilizowekwa na tume na hajasema juu ya kufanyika kwa mdahalo huu Oktoba 15.

Latest News

“TUTAJIRIDHISHA KABLA YA KUKUBALI CHANJO YA CORONA”- Rais Samia.
14 May 2021 18:24 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kupokea chanjo ya virusi vya Corona ni lazi [ ... ]

SOMALIA YATANGAZA KUREJESHA UHUSIANO NA KENYA.
06 May 2021 17:57 - Grace Melleor

Somalia imetangaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo m [ ... ]

KENYA NA TANZANIA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA.
05 May 2021 15:39 - Grace Melleor


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya pamoja na kuondoa vikwazo visivy  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.