Star Tv

Wagombea nafasi ya Makamu wa rais nchini Marekani Kamala Harris wa chama cha Democratic na Mike Pence wa Republicans hatimaye wamepata nafasi ya kufanya mdahalo wa pamoja kwa njia ya televisheni.

Hatua hiyo ya mdahalo huo wa wawili hao ni kuelekea Uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika tarehe tatu mwezi Novemba, lengo la mdahalo huo ni kutafuta uungwaji mkono kwa wafuasi wao, wakigusia masuala mbalimbali yanayolikumba taifa hilo.

Kinyume na mdahalo wa kwanza kati ya wagombea urais Joe Biden na Donald Trump uliotawaliwa na majibizano makali wiki iliyopita, Kamala na Pence walionekana watulivu.

Aidha, Bi. Harris ametumia mdahalo huu kuushtumu utawala wa Trump kwa kushindwa kukabiliana na janga la Corona ambalo limewaambukiza watu zaidi ya Milioni Saba nchini humo.

Hata hivyo, Pence amekanusha madai hayo na kusema utawala wake na Trump umefanya vya kutosha kukabiliana na janga hilo na kuongeza kuwa wapinzani wao wanatia siasa katika makabiliano dhidi ya janga hili.

Mdahalo huu uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Utah, umetangulia Mdahalo mwingine kati ya Trump na Biden hivi karibuni, kuendelea kuwaomba Wamarekani kuwapigia kura.
Uchaguzi wa urais wa Marekani umepangwa kufanyikja Novemba 3, 2020.

Latest News

“TUTAJIRIDHISHA KABLA YA KUKUBALI CHANJO YA CORONA”- Rais Samia.
14 May 2021 18:24 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kupokea chanjo ya virusi vya Corona ni lazi [ ... ]

SOMALIA YATANGAZA KUREJESHA UHUSIANO NA KENYA.
06 May 2021 17:57 - Grace Melleor

Somalia imetangaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo m [ ... ]

KENYA NA TANZANIA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA.
05 May 2021 15:39 - Grace Melleor


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya pamoja na kuondoa vikwazo visivy  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.