Star Tv

Wafanyakazi zaidi katika ikulu ya Marekani wamepatikana na virusi vya corona.

 Wafanyakazi hao wamegundulika ikiwa tu ni siku chache tu baada ya rais Donald Trump kulazwa hospitalini baada ya kupatikana na virusi hivyo.

Baadhi ya wafanyakazi wa hivi punde kuambukizwa ni pamoja na, mshauri mkuu katika ikulu ya White House, Stephen Miller, ambaye amekuwa karantini kwa siku chache zilizopita, na afisa mkuu katika jeshi.

Aidha, kwa sasa, Jenerali wa juu wa Marekani Mark Milley na viongozi wengine wa kijeshi wamejitenga baada ya Charles Ray kupatikana na maambukizi hayo.

Wakati hayo yakijiri, kati ya maafisa waliohudhuria mikutano na Charles Ray wiki iliyopita ambao kwa sasa wako karantini, hakuna mmoja wao ambaye amethibitika kuwa na maambukizi hayo au hata kuonesha dalili zozote za ugonjwa huo

 

Latest News

ETHIOPIA YASEMA HAITISHWI NA TAMKO LA RAIS DONALD TRUMP.
24 Oct 2020 16:54 - Grace Melleor

Waziri mkuu wa Ethiopia amesema nchi yake "haitakubali vitisho vya aina yoyote" baada ya Rais Donald Trump kusema kuwa M [ ... ]

RAIS TSHISEKEDI ATANGAZA MASHAURIANO YA UMOJA KWA MUUNGANO TAWALA.
24 Oct 2020 06:41 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, katika hotuba yake kwa taifa aliyoitoa siku ya Ijumaa wiki hi [ ... ]

SEKTA YA AFYA NCHINI YAPATA NEEMA KUTOKA USWISI.
23 Oct 2020 15:23 - Grace Melleor

Serikali imepokea msaada wa Faranga za Uswisi Milioni 15.75 sawa na shilingi Bilioni 39.59 kwa ajili ya kugharamia mradi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.