Star Tv

Rais wa Marekani Donald Trump anaendelea kupewa uangalizi wa karibu akiwa hospitali ambako anapokea matibabu ya ugonjwa wa Covid-19.

Kuna hali ya wasiwasi kuhusu uwezekano wa Rais Trump kutolewa hospitali,kama walivyokuwa wamesema madaktari wake kwamba huenda akatoka Jumatatu huku maswali yakiibuliwa kuhusu hali yake.

Kiwango cha oksijeni yake kilielezwa kushuka mara mbili na pia anatiliwa tiba ya steroid, Lakini siku ya Jumapili aliushangaza umma alipoonekana hadharani akiendeshwa kwenye gari kuwasalimu wafuasi wake, hatua ambayo ilikosolewa vikali.

Rais Trump, ambaye amekosolewa kwa jinsi alivyoshughulikia na janga la corona, pia alisema amejifunza mengi kuhusu virusi hivyo, Awali madaktari wake walisema Trump anaendelea kupata nafuu na kwamba huenda akatolewa hospitalini leo Jumatatu.

Dk Sean Conley alisema kiwango cha hewa ya oksijeni cha rais kilishuka mara mbili tangu alipogunduliwa kuwa na virusi vya corona, na ameanza kutumia dawa inayofahamika kama dexamethasone.

“Rais aliongezewa oksijeni ya ziada mara moja baada kuthibitishwa kuwa na virusi”- alisema Dk Conley, ambaye pia alifafanua mkanganyiko uliosababishwa na taarifa tofauti kuhusu hali ya Rais Trump.

Kuugua kwa Rais Trump kulikotangazwa hadharani na yeye mwenyewe kwenye mtandao wa Twitter mapema Ijumaa, kumevuruga ratiba yake ya kampeni.

Rais Trump atakabiliana na mpinzani wake wa chama cha Democratic Joe Biden katika uchaguzi wa urais wa Novemba tatu.

Latest News

ETHIOPIA YASEMA HAITISHWI NA TAMKO LA RAIS DONALD TRUMP.
24 Oct 2020 16:54 - Grace Melleor

Waziri mkuu wa Ethiopia amesema nchi yake "haitakubali vitisho vya aina yoyote" baada ya Rais Donald Trump kusema kuwa M [ ... ]

RAIS TSHISEKEDI ATANGAZA MASHAURIANO YA UMOJA KWA MUUNGANO TAWALA.
24 Oct 2020 06:41 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, katika hotuba yake kwa taifa aliyoitoa siku ya Ijumaa wiki hi [ ... ]

SEKTA YA AFYA NCHINI YAPATA NEEMA KUTOKA USWISI.
23 Oct 2020 15:23 - Grace Melleor

Serikali imepokea msaada wa Faranga za Uswisi Milioni 15.75 sawa na shilingi Bilioni 39.59 kwa ajili ya kugharamia mradi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.